Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Dkt. Semistatus H. Mashimba leo Jumanne Juni 9,2024 ametembelea Kata ya Kagera Nkanda kukagua miundombinu hasa ya shule za msingi kuona ni jinsi gani inaweza kuboreshwa.
Ambapo kupitia ziara hiyo alitembelea shule za msingi za Mvinza, Songambele, Nyanzanza pamoja na Shule ya Sekondari Kimenya.
Akizungumza katika tukio hilo Dkt. Mashimba amebainisha kuwa kata hiyo ina kaya zaidi ya 200,000 kitu kinachopelekea uhitaji wa watoto kwenda shule kuwa mkubwa hivyo kufika kwake kumelenga kuweka mipango ya baadae ya kuboresha miundombinu ya ufundishaji katika kata hiyo.
“Darasa moja kwa shule za msingi inatakiwa wanafunzi 60 na sekondari 40 hadi 45 lakini kwenye madarasa idadi hiyo imezidi kwahiyo tunatakiwa kuwekeza kwa kiasi kikubwa kwenye miundombinu ya madarasa na vyoo ili iwe rafiki kwa watoto kwa ajili ya kujisomea,” amesema.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.