Wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kujituma katika utendaji kazi ili kutengeneza mazingira wezeshi kwa halmshauri kukusanya mapato ya kutosha.
Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa halmshauri hiyo, Dkt. Semistatus H. Mashimba alipofanya kikao chake cha kwanza na wakuu hao wa idara na vitengo ambacho alikitumia kujitambulisha.
“Najua kabisa ‘resources zilizopo ni chache kwa maana ya fedha na miundombinu mingine hivyo ni lazima tuishi kwa upendo… na ili tuishi kwa upendo ni lazima tujitume katika kutengeneza mazingira ambayo yatatuingizia kipato ili tuwe na furaha,” amebainisha.
Aidha, amesema kuwa jukumu lake la kwanza kama kiongozi wa taasisi ni kuhakikisha inapofika mwishoni mwa mwezi wa tano halmashauri hiyo iwe inaongoza kwenye ukuanyaji wa mapato katika Mkoa wa Kigoma hivyo atalitilia mkazo suala hilo.
“Maelekezo ya sasa ya Mhe. Rais ni kuziona halamshauri zinakusanya mapato ya kutosha ili ziweze kuji ‘accommodate’ katika shughuli zinazoendelea… kwahiyo ndugu zangu tukae mguu sawa kila idara itawajibika katika zoezi la ukusanyaji wa mapato,” amebainisha.
Pia, amewataka wakuu hao wa idara na vitengo kuhakikisha wanatoa mrejesho wa maelekezo wanayoyapata kutoka sehemu mbalimbali.
Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi na Awali wa halmshauri hiyo, Elistina Chanafi amempongeza Mkurugenzi kwa msisitizo alioutoa wa ufanyaji kazi kama timu kitu anachoamini kitasaidia halmashauri kusonga mbele kwa haraka.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.