Mkurugenzi wa halmashauri ya Kasulu Mhandisi. Godfrey Kasekenya, akitoa ufafanuzi kwa wajumbe(hawapo pichani) kabla ya kuanza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Maendeleo Wilaya kujadili Mpango na Bajeti kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 kilichofanyika leo tarehe 25/2/2019 kwenye ukumbi wa Halmashauri.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali. Simon Anange akisisitiza jambo, wakati akifungua kikao cha Kamati ya Ushauri ya Maendeleo wilaya, kujadili Mapitio ya Mpango na Bajeti kwa mwaka wa Fedha 2019/2020.
Mwakilishi toka Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wilayani Kasulu Ndg. Michael Bisama, akichangia hoja. Mashirika mbalimbali pamoja na Taasisi zisizo za Kiserikali ni wadau Muhimu katika kuchangia Bajeti ya Halmashauri ya wilaya ya Kasulu.
Na.Andrew Ginnethon.
Kikao cha Kamati ya ushauri ya Maendeleo Halmashauri ya wilaya ya Kasulu, kimepitia Mapitio ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2017/2018,2018/2019 na Makisio na kupitisha Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 wilayani hapa.
Akifungua Kikao hicho, Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali. Simon Anange amewataka wajumbe kutoa ushauri na mawazo yenye tija kuhusu Mpango na Bajeti hiyo kwa lengo la kuboresha huduma kwa Jamii.
Aidha ameyataka Mashirika yanayotoa huduma kwa wakimbizi waliopo wilayani hapa, kujielekeza katika kuisaidia Jamii ya wakazi wenyeji ambao wanaathiriwa kiasi kikubwa na uwepo wa Wakimbizi hao.
“Mashirika mengi yameshindwa kuisaidia Jamii kwa kutoa misaada yenye tija kwa wananchi bali imekuwa ikitolewa misaada isiyo endelevu ambayo manufaa ya muda mrefu kwa wakazi wanaozunguuka maeneo wanayoishi wakimbizi” amesema Anange.
Akizungumza na wadau wa Mkutano huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kasulu Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema uwepo wa wadau wa maendeleo ni muhimu ili kufahamu watachangia kiasi gani katika Bajeti hiyo.
Ameshauri kuwa, Mashirika mbalimbali yanapotoa misaada ni lazima yawasiliane na Halmashauri ili kuepuka kutekeleza mpango mmoja kwa pamoja na badala yake Halmashauri ijielekeze kwenye utekelezaji mipango mingine.
Akiwasilisha Makisio ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2019/2020, Afisa Mipango Takwimu na Ufuatiliaji wa Wilaya Ndg. Jackob Kilatu, amesema halmashauri imekisia kutumia zaidi ya Shilingi Bil 48.2 katika kutekeleza Miradi mbalimbali na uendeshaji wa Halmashauri.
Ndg. Mbela Abdallah, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya, amepongeza maandalizi mazuri na mchakato mzima uliofanywa na wataalam kwa kushirkikana na Mkurugeni hali iliyopelekea Mpango na Bajeti hiyo kufikia hatua iliyopo.
Akishangia Mapendekezo ya Mpango na Bajeti, katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilaya Ndg.Rajabu Bujoro ameshauri kwenye Bajeti ijayo, uwepo mkakati mkubwa wa utunzaji wa Mazingira pamoja na vyanzo vya Maji.
Wajumbe walihitimisha kikao kwa kauli moja ya kuukubali na kuupitisha mpangona huo kwa lengo la Maendeleo ya wilaya ya Kasulu na Taifa kwa ujumla katika kuhakikisha huduma inawafikia wananchi katika ubora.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.