Na Mwandishi Wetu
Leo Jumatatu Machi 24,2025, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu,Mhe. Kanali Isaac Mwakisu,amewasilisha taarifa muhimu kuhusu Utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mpinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025 ya Wilaya ya Kasulu katika kipindi cha kufikia mwezi Februari mwaka huu.
Katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Kasulu Mji, Kanali Mwakisu ameeleza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta mbalimbali,ikiwa ni pamoja na ongezeko la upatikanaji wa umeme,elimu na huduma za afya.
Amesema mitaa 108,vijiji 61, na vitongoji 222 vimepatiwa umeme ikiwa ni ongezeko la 81.32% ya upatikanaji wa huduma hiyo, na sekta ya elimu msingi imejenga madarasa mapya 236 na shule mpya 15.
“Sekta ya elimu sekondari imejenga madarasa mapya 338,shule mpya 11,ukamilishaji wa madarasa 39,ukamilishaji wa maboma 33,ukamilishaji wa mabweni 12,maabara ya sayansi 23,nyumba za walimu 7,mabweni mapya 12,vyoo matundu 200 na viti na meza jozi 4680,” amesema Kanali Mwakisu.
Aidha, amesema kuwa katika sekta ya afya kuna ongezeko la upatikanaji wa dawa, vifaa tiba,vitendanishi na vifaa saidizi kutoka 83.11% hadi 90.6% pamoja na kaya zinazotumia vyoo kuongezeka kutoka 63.85% hadi 99.8%..
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kasulu, Mbelwa Chidebwe amaetoa pongezi kwa watumishi wa wilaya hiyo kwa juhudi wanazofanya katika usimamizi wa miradi kitu kilichosaidia utekelezaji wa ilani ya chama kuwa rahisi kwa kuyafanyia kazi maelekezo yote yanayotolewa.
Katika kuelekea uchaguzi ujao, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kigoma, Zaituni Buyogera,amesisitiza umuhimu wa kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ili wananchi waweze kutumia haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanaowataka.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.