Na Mwandishi Wetu
Wamiliki wa vyombo vya habari na waandishi wa habari Mkoani Kigoma wametakiwa kushirikiana na Jamii katika kukuza Viwango vya elimu Mkoani hapo
Wadau hao wa habari wametakiwa na Katibu Tawala Msaidizi idara ya elimu Mkoa wa Kigoma Bi. Paulina Ndigezà akimuwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa huo January 16, 2023 katika kikao kilichofanyikia Ukumbi wa Hoteli ya Glonency uliopo Halmashauri ya Mji Kasulu
Kikao hicho kilihusisha Wamiliki wa Vyombo vya habari, Maafisa Mawasiliano Serikalini, Maafisa elimu ngazi ya Mkoa , na Waandishi wa Habari waliopo Mkoani hapo
Katika kikao hicho kiongozi huyo aliwataka wadau hao wa vyombo vya habari kuendelea kutoa taarifa na elimu kwa umma juu ya miradi inayotekelezwa Mkoani hapo ikiwemo mradi wa Shule Bora
Aliendelea kuwataka kuelimisha jamii kushiriki kwa kuzifanya Shule ziwajibike na kuongeza uelewa wa Jamii kuhusu umuhimu wa kila Mtoto( Kike au Kiume), na Watoto wenye ulemavu kuandikisha na kuhudhuria Shule
Awali akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji Afisa habari wa Mradi wa Shule Bora Ndugu. Raymond kayombo alisema mradi wa Shule bora umekuwa ukitekeleza mafunzo ya Walimu kazini (MEWAKA) kwa lengo la kuboresha suala la Ufundishaji na Ujifunzaji
Aidha amesema tayari Maafisa Mawasiliano Serikalini kwa ngazi ya Mikoa na Halmashauri inayotekeleza mradi wamefanya vikao na kuweka maazimio namna watakavyofanya kazi na Wamiliki wa vyombo vya habari pamoja na Waandishi wa Habari katika kuboresha utoaji wa taarifa za mafanikio
Alisema katika utekelezaji wa mradi wa Shule bora Wajibu wa Wamiliki wa vyombo vya habari na waandishi wa habari ni kuibua changamoto na uelimishaji wa jamii katika maeneo yanayotekelezwa na mradi ikiwemo suala la Ufundishaji , Mazingira salama ya kujifunzia, Elimu jumuishi, Ufaulu na Mdondoko wa wanafunzi
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais TAMISEMI Ndugu. Fred Kibano aliwataka Waandishi wa Habari kutumia kalamu zao kufikisha ujumbe kwa jamii kupitia Uandishi wa Habari, makala, uandaaji wa vipindi kupitia vyombo vyote vya habari ikiwemo magazaeti, radio, televisheni, na mitandao ya kijamii ili kufikisha ujumbe kwa makundi mbalimbali
Naye Katibu Msaidizi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Kigoma Ndugu. Jackson Ruvilo alisema Waandishi wa habari wataendelea kushirikiana na Serikali kupitia Mradi wa Shule Bora kuhabarisha na kuelimisha jamii kuhakikisha Watoto wanapata elimu bora kupitia Wadau mbalimbali wakiwemo Jamii, Wazazi, Walimu na Mamlaka zinazosimamia elimu Mkoani hapo
Miradi wa Shule bora unatekelezwa katika Mikoa tisa (9) Nchini Tanzania ukihusisha Halmashauri sitini na saba (67) na Shule elfu tano mia saba hamsini na saba ( 5, 757) na Unatarajia kuwanufaisha Wanafunzi zaidi ya Milioni tatu na laki nane ( 3, 800,000) na Walimu zaidi ya elfu hamsini na nne ( 54, 000)
Mikoa inayotekeleza mradi wa Shule bora ni pamoja na Mkoa wa Kigoma, Katavi, Dodoma, Mara, Pwani, Rukwa, Simiyu, Singida na Mkoa wa Tanga
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.