Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mhe. Balozi Simon Sirro, leo Jumanne Julai 8,2025 ametembelea Kiwanda cha Sukari Kasulu kujionea maendeleo ya ujenzi na upandaji miwa, ambapo ameonesha kuridhishwa na hatua iliyofikiwa. Ametaja kuwa kiwanda hicho kinatarajiwa kuanza kazi 2027 na tayari kimetoa ajira kwa watu 500, wakiwemo 109 wenye weledi wa fani tofauti. Amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kukuza viwanda na kupunguza changamoto ya ajira, huku akiwakaribisha wawekezaji akisema Kigoma sasa ina miundombinu bora zaidi kuliko zamani.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.