Na Mwandishi Wetu
Katibu Tawala (RAS) Mkoa wa Kigoma, Hassan Rugwa amefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu.
Ambapo amepongeza namna halamshauri hiyo ilivyoweza kutekeleza maagizo yake aliyotoa hivi karibuni ya kufanyika marekebisho madogo madogo katika jengo jipya la utawala pamoja na kuanza kufanya kazi kwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Wilaya.
Pamoja na kuelekeza spidi ya ujenzi wa Zahanati ya Chekenya iongezwe ili kuwasogezea karibu wananchi wa eneo hilo huduma za afya.
“Mfanye mawasiliano ya mapema na watu wanaohusika na uwekaji wa miundombinu ya umeme na maji ikiwemo kuwaeleza ni lini zahanati hiyo itafunguliwa ili ikianza kufanya kazi huduma hizo ziwepo,” amesema.
Katika hatua nyingine Rugwa ameagiza maeneo yote ya serikali katika halmashauri hiyo yanayotekeza miradi ya maendeleo kupangwa na kupimwa ili yaweze kutambulika kisheria ili kuepuka uvamizi siku za mbeleni.
Katika ziara hiyo miongoni mwa miradi iliyopata fursa ya kutembelewa ni pamoja na ujenzi wa Zahanati ya Chekenya, jengo jipya la utawala la makao makuu na chumba cha upasuaji cha Hospitali ya Wilaya ya halmashauri hiyo.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.