Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kutekeleza kwa vitendo dhamira yake ya kuufungua Mkoa wa Kigoma ikiwemo kuufanya kuwa kitovu cha Biashara ukanda wa mikoa ya Magharibi.
Dkt. Nchimbi amesema hayo alipokuwa anazungumza na wakazi wa Wilaya ya Kasulu kwenye ziara yake mkoani humi aliyoambatana na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM Taifa.
Amesema Rais Dkt. Samia ametoa zaidi ya Shilingi Tril. 11 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya kijamii sambamba na ile yenye kuwawezesha wananchi kiuchumi.
"Kuna hatua kubwa ya kimaendeleo imefikiwa hapa mkoani Kigoma katika utekelezaji wa miradi ikiwemo ujenzi wa barabara, ukarabati wa meli, upanuzi wa uwanja wa ndege, sambamba na miradi mbalimbali ya kutolea huduma za jamii, hizi zote ni kazi nzuri zinazotekelezwa na serikali ya awamu ya sita mkoani hapa," amesisitiza.
Katika hatua nyingine Dkt. Nchimbi ameiagiza Wizara ya Nishati kufuatilia na kutatua changamoto ya huduma ya Umeme wilayani Kasulu.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.