Na Mwandishi Wetu
Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma, leo Jumanne Julai 15, 2025, imefanya kikao kazi maalum katika Ukumbi wa Kagoma, Makao Makuu ya Halmashauri, kwa ajili ya maandalizi ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kupokelewa rasmi Septemba 17, 2025. Kikao hicho kilichoongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri, Ndelekwa Vanica, kimewakutanisha Wakuu wa Divisheni na Vitengo, Watendaji wa Kata pamoja na Wajumbe wa Kamati mbalimbali, ambapo wamejadili kwa pamoja mikakati madhubuti ya kuhakikisha mapokezi hayo yanakuwa ya mafanikio kwa kuzingatia ushirikiano, uwazi na ushirikishwaji wa wananchi, sambamba na kuutumia Mwenge wa Uhuru kama fursa ya kuhamasisha maendeleo endelevu katika Wilaya ya Kasulu.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.