• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

RC SIRRO AITAKA KASULU KUTENGA MAENEO KWA AKILI YA UWEKEZAJI

Posted on: July 8th, 2025

Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mhe. Balozi Simon Sirro, amezitaka halmashauri zote zilizopo katika Wilaya ya Kasulu kuhakikisha zinatenga maeneo mahususi kwa ajili ya uwekezaji, ili kuwawezesha  kupata maeneo kwa urahisi bila vikwazo.

Balozi Sirro ametoa wito huo leo Jumanne, Julai 8, 2025, wakati wa ziara yake ya kujitambulisha kwa viongozi wa Serikali, watumishi, wananchi, viongozi wa dini na wazee maarufu, iliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu.

“Nafahamu wilaya yetu ina fursa nyingi za uwekezaji kupitia kilimo cha mazao ya chakula na biashara, pamoja na utalii. Nisisitize tu watendaji kuongeza ubunifu na kuweka mifumo mizuri ya usimamizi, sambamba na kutoa ushirikiano kwa wawekezaji waliopo na watakaoingia ili kuongeza pato la wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla,” amesema.

Aidha, kutokana na mkoa huo kupakana na baadhi ya nchi zenye changamoto za kiusalama, Balozi Sirro amehimiza watumishi wa umma kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ili kuhakikisha wageni wanaoingia nchini wanazingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo kwa lengo la kudumisha amani na utulivu.

Katika hotuba yake, amesisitiza umuhimu wa watendaji kuzingatia vipaumbele vya mkoa, ikiwemo usimamizi wa miradi ya maendeleo, utekelezaji wa sera ya matumizi bora ya ardhi, kukuza biashara na uwekezaji, kuibua vyanzo vipya vya mapato, pamoja na kuboresha huduma za elimu, afya na maji.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Mhe. Kanali Isaac Mwakisu, amesema kuwa hali ya usalama katika wilaya hiyo ni shwari, na kwamba maeneo ambayo tayari yamechukuliwa na wawekezaji wakubwa yatalindwa kwa gharama yoyote ili kuendeleza hamasa ya uwekezaji zaidi.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, akizungumza kwa niaba ya wananchi, amesema kuwa wao kama wawakilishi wa majimbo ya Kasulu wanajivunia mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala, ambayo imeleta maendeleo makubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • RC SIRRO ARIDHISHWA NA MAENDELEO KIWANDA CHA SUKARI KASULU,ATAJA AJIRA 500 TAYARI ZIMETOLEWA

    July 08, 2025
  • RC SIRRO AITAKA KASULU KUTENGA MAENEO KWA AKILI YA UWEKEZAJI

    July 08, 2025
  • MAAFISA ELIMU WATAKIWA KUTATHMINI MATOKEO YA MTIHANI WA MOKO

    July 02, 2025
  • KASULU YAWEZESHA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU KWA MIKOPO YA MILIONI 870

    June 20, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.