Na Mwandishi Wetu
Maafisa elimu kata na walimu wakuu wa shule za msingi Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu wametakiwa kufanya tathmini ya Mtihani wa Moko ili kuwatambua wanafunzi waliopata alama za chini na kuweka mikakati ya kuwawezesha kuongeza ufaulu.
Akizungumza kwenye kikao cha tathmini ya elimu leo Julai 2, 2025, Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri hiyo, Elestina Chanafi, amesisitiza umuhimu wa kusaidia wanafunzi waliopata alama D na E kufikia C hadi A.
Aidha, amewataka walimu wakuu na maafisa elimu kuhakikisha matumizi sahihi ya mifumo ya serikali katika maeneo ya taaluma, utumishi, na fedha. Amesisitiza umuhimu wa kusimamia miradi inayoendeshwa mashuleni ili ikamilike kwa wakati na kuonyesha thamani halisi ya fedha zinazotumika.
Naye Afisa Uthibiti Ubora wa Shule, Leonsia Sugwejo, amesema tathmini kwa njia ya video imeonyesha mafanikio makubwa, ikiwemo kuibuka kwa Mwalimu Joseph Masika wa Shule ya Sekondari Kitanga kuwa miongoni mwa washindi wa juu kitaifa kwenye somo la Fizikia.
Afisa Ajira na Maendeleo ya Walimu (TSC) Wilaya ya Kasulu, Kazimoto Nkomoli, amewataka walimu kuzingatia matumizi sahihi ya mfumo wa E-Utendaji ili kuepuka madhara ya kutotambuliwa kiutumishi au kukosa fursa za maendeleo.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa Shule Bora Mkoa wa Kigoma, Celestine Bukango, amehimiza shule kuwa na dira ili kuhakikisha shughuli zote zinaendeshwa kwa mwelekeo thabiti unaoakisi malengo ya shul
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.