Watumishi wa kada ya Afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu wametakiwa kujifunza na kuelewa vifaa vya kieloktroniki ili waweze kuendana na kasi ya teknolijia.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Halmashauri hiyo Robert Rwebangira alipokuwa anafungua mafunzo ya Mfumo wa Kielektroniki wa GoT-HOMIS kwa watumishi wa kada hiyo leo Jumatatu Agosti 5, 2024
Ameeleza kuwa Mfumo huo umewekwa kwa lengo mahususi ili kusimamia shughuli za uendeshaji wa vituo vya kutolea huduma za afya.
Pia, amesema kuwa mfumo huo utasaidia kupunguza malamiko kutoka kwa wagonjwa pamoja na utunzaji mzuri wa kumbukumbu katika vituo vya afya na zahanati.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.