Na Waandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Isaac Mwakisu amesema kuwa kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Disemba 2023 wamepokea fedha zaidi ya shilingi bilioni 171 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo.
Mwakisu ameyabainisha hayo jana alipokuwa anawasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Disemba 2023 kwa wajumbe wa halmashauri kuu wa chama hicho wilayani humo.
“Miongoni mwa hizo fedha zimetoka serikali kuu, wahisani na makusanyo ya mapato ya ndani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu na Kasulu Mji na kuelekezwa katika tasnia ya elimu, maji, miundombinu ya barabara kwa maana ya Tarula, umeme lakini pia kwenye afya,” amesema.
Amesema uwasilishaji huo umefanyika ili wajumbe wapate kujua nini kimefanyika kwa kipindi hicho kupitia ilani ya chama chao kwa kuwaonyesha vitu vyote vilivyotekelezwa.
Aidha, Mwakisu amewataka wananchi wa wilaya hiyo kujiepusha na vitendo vya ramli chongani maarufu kama Kamchape au Lamba lamba kwakuwa ni vitendo vinavyozua taharuki na kuhatarisha usalama wa watu.
“Athari ni nyingi kupitia ramli chonganishi kwa mwananchi anayetuhumiwa kuwa ni mchawi kutengwa na wenzake kwa kuonekana si mtu wa kawaida, sisi kama serikali tunakemea hayo pamoja na kutoa elimu ili watu wasiwe na akili kwamba kamchape ndio mkombozi wao,” amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kasulu, Mbelwa Chidebwe amesema chama hicho hakiungi mkono masuala ya ramli chonganishi kwakuwa tayari wameshajiridhisha kuwa wanaofanya vitendo hivyo ni kundi la wahuni na matapeli.
“Zamani kumpata Kamchape ilikuwa ni shida na walikuwa wanafanya kazi zao usiku ila hawa wa sasa ni wezi tunaamini serikali haina dini ila wananchi wake wana dini hivyo kila mmoja kwa imani yake akafanye maombi kwa jili ya kutokomeza vitendo hivi,” amebainisha.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.