• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

KASULU DC YAANZISHA SHAMBA DARASA LA VIAZI LISHE KUKABILIANA NA UTAPIAMLO

Posted on: June 15th, 2025

Na Mwandishi Wetu 

Katika jitihada za kukabiliana na changamoto ya utapiamlo na lishe duni, Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, kupitia Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, imeanzisha shamba darasa la viazi lishe katika Hospitali ya Wilaya. Lengo kuu ni kuwafundisha kina mama wanaohudhuria Kliniki ya Baba, Mama na Mtoto (RCH) kuhusu umuhimu wa viazi hivyo na namna bora ya kuvilima.

Viazi lishe, ambavyo ni chanzo kizuri cha Vitamini A, husaidia watoto kuwa na afya bora, kuimarisha nguvu na kinga ya mwili, kuzuia upofu utotoni, kupunguza hatari ya vifo vya watoto wachanga, na kushusha viwango vya upungufu wa damu mwilini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shamba hilo hospitalini hapo, Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri, Mikidadi Mbaruku, amesema kuwa iwapo wananchi watahamasika kulima zao hilo, serikali itapunguza matumizi ya fedha kununua matone ya vitamini A, fedha ambazo zinaweza kuelekezwa kwenye shughuli nyingine za maendeleo.

“Idara ya Kilimo tumeamua kuanzisha shamba hili hapa hospitalini ili kina mama mnapofika kliniki au kwa ajili ya matibabu, muweze kujifunza namna viazi hivi vinavyolimwa. Pia tunawahimiza wote wanaohitaji mbegu kuwasiliana na maafisa ugani katika vijiji vyao ili waelekezwe vizuri kuhusu upandaji na matumizi ya viazi hivi,” amesema Mbaruku.

Kwa upande wake, Afisa Lishe wa Halmashauri hiyo, Subira Swai, amesema matumizi ya viazi lishe yatapunguza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa vidonge vya virutubisho, na kuwataka wakina mama wanaohudhuria kliniki kutumia vyema wataalamu wa kilimo waliopo kwa ushauri.

Naye Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu,  Masumbuko Kwelema, amewahimiza kina mama wajawazito na wale wenye watoto wachanga kuhakikisha wanakuwa na bustani za viazi hivyo majumbani mwao kama njia mojawapo ya kuboresha lishe na afya ya familia.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • KASULU DC YAANZISHA SHAMBA DARASA LA VIAZI LISHE KUKABILIANA NA UTAPIAMLO

    June 15, 2025
  • KUU KASULU YAKAGUA MIRADI YA MWENGE

    June 13, 2025
  • MATUMIZI YA ZANA ZA UFUNDISHAJI YATAJWA KUONGEZA UFANISI SHULENI

    June 11, 2025
  • WALIMU SHULE YA MSINGI KISUMA WATOA SHUKRANI KWA WADAU WALIOCHANGIA SARE NA VIFAA KWA WANAFUNZI

    June 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.