Na Mwandishi Wetu
Kadi za mpiga kura zilizotolewa 2015 na 2020 zitaendelea kutumika katika chaguzi zijazo bila kujali mabadiliko ya jina kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Hayo yamebainishwa leo Jumatatu Julai 22,2024 na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,Kailima Ramadhan alipofanya ziara katika vituo vya kuandikisha wapiga kura kwenye Halmshauri ya Wilaya ya Kasulu.
"Naomba nitoe wito kwa wale ambao kadi zao ni zile zenye jina la Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kudhani kubadilika kwa jina la tume wanatakiwa wabadili kadi watambue kuwa kadi zao ni halali kwa mujibu wa kifungu cha 168 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani Na 1 ya Mwaka 2024," amesema.
Pia, amewakumbusha wananchi wa mikoa ya Kigoma Tabora na Katavi kuwa zimebaki siku nne kabla ya zoezi hilo kukamilika , hivyo wajitokeze kwa wingi ili kuzitumia vizuri siku hizo.
Uboreshaji wa Daftari kwenye mikoa hiyo umeanza Julai 20,2024 na utafanyika kwa siku saba hadi Julai 26,2024 huku vituo vya uandikishaji vikifunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.