• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

WAZAZI NA WANAFUNZI WATAKIWA KUWA MABALOZI KWENYE ZOEZI LA UANDIKISHAJI

Posted on: October 3rd, 2024

Na Mwandishi Wetu 

Wazazi na wanafunzi walioudhuria Mahafali ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari  Nkundutsi  iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kuwa mabalozi katika kuhamasisha umma kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura zoezi linalotarajiwa kuanza Oktoba 11, 2024 na kufikia tamati mnamo Oktoba 20,2024.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu, Theresia Mtewele leo Alhamisi Oktoba 3,2024 alipokuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo na kubainisha kuwa kwa kufanya hivyo itasaidia kupata viongozi sahihi wa Serikali za Mitaa wenye kubeba dhamana ya maendeleo katika maeneo yao.

“Tukiwa tunaelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 maandalizi yameiva ninahamasisha wananchi wote mliopo hapa na wahitimu mliofikisha umri wa miaka 18 muende mkajiorodheshe kwenye daftari la kupiga kura tupate viongozi watakaoharakisha maendeleo yetu kwa mustakabali mzima wa taifa letu,” amesema.

Aidha, Theresia amewataka  wanafunzi wanaondelea na masomo katika shule hiyo kutia bidii katika masomo baada ya wenzao kuhitimu ili kuhakikisha ufaulu unaongezeka kitu kitakachosaidia jina la shule hiyo kupaa maeneo tofauti hapa nchini.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Focus Albert amehimiza wazazi ambao watoto wao watachaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza hapo mwakani kuhakikisha wanaripoti mashuleni na kuwafuatilia mwenendo wao ili waweze kumaliza hadi kidato cha nne.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo, Dunstan Munyungu matarajio yao ni kufuta matokeo ya sifuri na kupunguza daraja la nne na mikakati tayari imewekwa katika kufanikisha hilo ndio maana wamekuwa shule ya kwanza kwenye mitihani ya kujipima kwa ngazi ya halmshauri.

Katika mahafali hayo ilishuhudiwa iadadi ya wahitimu 95 ambapo wavulana  ni 45 na wasichana ni 50.


Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • KASULU DC YAANZISHA SHAMBA DARASA LA VIAZI LISHE KUKABILIANA NA UTAPIAMLO

    June 15, 2025
  • KUU KASULU YAKAGUA MIRADI YA MWENGE

    June 13, 2025
  • MATUMIZI YA ZANA ZA UFUNDISHAJI YATAJWA KUONGEZA UFANISI SHULENI

    June 11, 2025
  • WALIMU SHULE YA MSINGI KISUMA WATOA SHUKRANI KWA WADAU WALIOCHANGIA SARE NA VIFAA KWA WANAFUNZI

    June 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.