Na Mwandishi Wetu
Watendaji wa kata katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kuhamasisha wananchi kwenye maeneo yao wafanye maandilizi mazuri ya mashamba msimu huu wa kilimo unapokaribia.
Kwa lengo la kuwawezesha kuvuna mazao mengi ili wanapoombwa kuchangia chakula mashuleni kusiwe na mgongano baina yao kwenye utekelezaji wake.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu, Theresia Mtewele ameyabainisha hayo jana Ijumaa Agosti 23,2024 wilayani humo kwenye Kikao cha Tathimini ya Mkataba wa Lishe ambapo alikuwa mgeni rasmi.
“Kwahiyo tuhamasishe wananchi tunaelekea msimu mpya wa kilimo waanze mandalizi mapema ili wananchi wapate mapato na mavuno mazuri ili ikifika wakati anatakiwa achangie chakula shuleni inakuwa rahisi,” amesema.
Aidha, amesisitiza kwa kata ambazo shule zake hazitoi chakula mashuleni hasa kwa madarasa ya mtihani watendaji wake kwenda kujifunza kwa wenzao ni namna gani wameweza kufanikiwa katika hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Emmanuel Ladislaus amesema kuwa mikakati iliyoelekezwa katika kikao hicho kama itafanyiwa kazi itakuwa njia mojawapo ya kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Sita iliyojikta kujenga taifa la watu wenye afya.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.