Wasichana wenye umri barehe walio katika mpango wa kuwawezesha wasichana unaofadhiriwa na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Sayansi, Elimu na Utamaduni UNESCO, wametakiwa kuwa wabunifu ili kuyafikia malengo yanayokusudiwa.Woto huo ulitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Joseph Kashushura alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tatu kwa washiriki wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Serengeti mapema mwezi uliopita.Kashushura anewataka pia washiriki wa mafunzo hayo kuachana na tabia ya kutumia changamoto kama kikwazo cha mafanikio yao na badala yake watumie teknolojia ya mawasiliano kuwasiliana na wenzao ili kufikia malengo.Mpango wa kuwazesha wasichana unatekelezwa katika Halmashauri tatu tu nchini zilizopo katika mikoa ya Arusha(Ngorongoro), Mwanza (Sengerema) na Kigoma (Kasulu).
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.