Wananchi wa Mkoa Wa Kigoma wamehaswa kupinga vitendo vya Rushwa na aina yoyote ya ubadhilifu ili kuhakikisha miaka 61 ijayo ya uhuru inakuwa ya matumaini na mafanikio kwani vitendo hivyo vinaleta maendeleo ya wasiwasi, ukamilishaji wa miradi kuwa wa shida na kutopatikana kwa haki za huduma za wananchi
Aliyasema hayo muwakilishi wa Mkuu Wa Mkoa Wa Kigoma Kanali Michael Masala Justine Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe alipokua akitoa salamu katika kongamano la maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika kimkoa Wilayani Kasulu.
“Serikali inaweka fedha nyingi kwaajili ya miradi ya maendeleo sisi sote ni wafaidika wa miradi hiyo tusiseme miradi hii ni ya viongozi tu kila mmoja awe muwajibikaji katika kusimamia miradi ya maendeleo, tupinge sana rushwa na vitendo vyovyote vya ubadhilifu ili kuhakikisha miaka 61 ijayo inakuwa ya matumaini na mafanikio” alisema kanali Massala
Kwa upande wake Katibu Tawala Wa Mkoa Wa Kigoma Albert Msovera aliwashukuru viongozi wa wilaya ya kasulu kwa maandalizi mazuri na kuipongeza serikali kwa jitihada mbalimbali inazoendelea nazo na kuongeza kuwa serikali inafanya mambo mengi makubwa na inavipaombele vingi hivyo haiwezi kufanyia kazi kila kitu kwa pamoja
Msovera aliongeza kuwa serikali ya Tanzania ni sikivu na inaendelea kufanya kazi kutokana na upatikanaji wa fedha na mipango ya serikali iliyopo na kuahidi kuwa changamoto zote na mapendekezo yatafanyiwa kazi, vilevile aliwahasa watumishi wa mkoani humo kusimama katika nafasi zao ili kutoa huduma stahiki kwa wananchi .
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu
Aidha Mkurugenzi Mtendaji Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Kasulu Joseph Kashushura alieleza kuwa serikali inautayari wa kuwasaidia wananchi wake katika miradi wanayoanzisha lakini kumekuwa na ukiukwaji wa taratibu za utekelezaji wa miradi hivyo kupelekea serikali kushindwa kufanya ukamilishaji wa miradi hiyo.
Aliongeza kuwa serikali inasaidia kukamilisha miradi kwa asilimia 100 kwakutoa shilingi 12,500,000/= katika ikamilishaji wa madarasa na 50,000,000/= kwa zahanati, licha ya nia nzuri ya wananchi walionayo kumekuwa na ukiukwaji wa Sheria, Taratibu Na Kanuni
Kashushura Aliwashauri Watendaji Na Waheshimiwa Madiwani kuhakikisha wanawaelewesha vyema wananchi juu ya utoaji wa taarifa na kufata utaratibu pindi wanapotaka kufanya shughuli yoyote ya maendeleo
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.