Na Mwandishi Wetu, Kasulu
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu, Theresia Mtewele amewataka wanafunzi wa shule za sekondari zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kuwa mabalozi wazuri kwenye kuhamasisha wazazi wao ili waweze kujitokeza wa wingi kwenye zoezi la uandikishaji wa vyeti vya kuzaliwa jwa watoto wenye umri wa siku 0-90.
Theresia aliyasema hayo jana alipokuwa kwenye ziara yake ya kutoa elimu na hamasa ya kujiandikisha kupata vyeti vya kuzaliwa katika shule za sekondari Kasangezi na Nkundusi zilizipo wilayani humo.
Ambapo amesema kuwa hamasa hiyo imelenga kusaidia dhima ya serikali inayotaka watanzania wote kuwa na vyeti vya kuzaliwa ifikapo mwaka 2030 kwa ajili ya kuweka takwimu sahihi ikiwemi kuweka mipango endelevu ya utoaji huduma stahiki kwa jamii.
“Tunajua nyinyi ni wababa na wamama watarajiwa naomba mlibebe hili katika hali ya ubalozi ili mkawaelimishe wazazi na walezi wenu umuhimu wa kuwa na cheti cha kuzaliwa ikiwemo kuwasaidia kuweka mahusiano ya matukio muhimu ya kibinadamu na katika ajira zenu katika siku za mbeleni”, amesema.
Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari wa halmashauri hiyo, Iyogo Isuja ambaye aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Dkt. Semistatus H. Mashimba amesema kuwa suals la kuwa na cheti cha kuzaliwa ni haki ya msingi kwa kila mtoto wa kitanzania.
Pia, amewashukuru wazazi waliojitokeza katika tukio hilo na kuwataka kuendelea kutoa ushirkiano katika zoezi hilo litakalowasaidia watoto wao kwenye kupata huduma tofauti katika jamii zao.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Jalali Kiumbe amewataka wazazi kujitokeza kwenye zoezi hilo lililolenga watoto wa umri huo kuhakikisha wanapata vyeti hivyo kwakuwa ni nyaraka muhimu kwa siku zao za maisha yao yao ya mbeleni.
Ambapo ameeleza kuwa zoezi la utoaji wa Vyeti vya Kuzaliwa lilianza Oktoba-Disemba mwaka 2023 kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 katika vituo vya kutolea huduma za afya na kwasasa zoezi hilo linaendelea kwa watoto wenye umri wa siku 0-90 kwenye utambuzi wa taarifa zao.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.