Na. Andrew Mlama-Kasulu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mha. Godfrey Kasekenya, amewaongoza Wakuu wa Idara na Vitengo katika ziara ya kukagua Maendeleo ya ujenzi wa Miundombinu ya Hospitali pamoja na kuzunguukia na kujionea eneo linalitarajiwa kujengwa makao makuu ya wilaya hiyo.
Akiwa katika eneo la Ujenzi wa Hospitali, Mha. Kasekenya amekagua maendeleo ya ujenzi wa majengo mbalimbali ikiwemo jengo la Wodi ya wazazi, Maabara, jengo la wagonjwa wa Nje, Stoo ya madawa, Jengo la Mionzi, usafi pamoja na Utawawala, ambapo ameonyesha kuridhishwa na kasi ya utendaji kazi pamoja na ubora wa majengo yanayoendelea kujengwa.
Aidha Mkurugenzi amewaongoza wakuu hao wa Idara na Vitengo kutembelea na kujionea eneo linalotarajiwa kujengwa Miundombinu mbalimbali kwa ajili ya makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu.
Amewasisitiza watumishi wa Idara ya Ardhi na Maliasili kuhakikisha wanakamilisha michakato muhimu itakayohalalisha matumizi ya Ardhi katika eneo hilo ikiwemo ujenzi wa Ofisi za Serikali, Kituo cha Mabasi, maeneo ya kibiashara, Kituo cha Polisi, Shule, Vyuo, uuzaji wa viwanja kwa watu binafsi nk.
Mtaalam wa Idara ya Ardhi Ndg. Abidius Boniface akifafanua jambo kwa Baadhi ya wakuu wa Idara.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mha. Godfrey Kasekenya akitolea ufafanuzi wa jambo kwa baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo wakati wa Ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Wilaya.
Mratibu wa TASAF wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Ndg. Almachius Njungani akiweka Saini kwenye kitabu cha wageni baada ya kukagua vifaa kwenye Stoo ya kuhifadhia vifaa vya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kasulu.
Muonekano wa Jengo la Wodi ya wazazi ambalo ni mojawapo wa Majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Kasulu, kazi ya upauaji ikiendelea na mafundi wakiwa kazini.
Baadhi ya wakuu wa Idara na vitengo wakiwa katika Picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mha. Godfrey Kasekenya (wa Tano kutoka kushoto) mara baada ya kuhitimisha ziara ya kukagua eneo linalotarajiwa kujengwa makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.