• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

WAKAZI KATA YA MAKERE WAWAJENGEA NYUMBA WASIO NA MAKAZI.

Posted on: August 28th, 2018


Na.Andrew Mlama-Kasulu.

Wakazi wa Kata ya Makere iliyopo wilayani hapa, wameamua kuwasaidia wenzao walio kwenye kaya duni  katika kuwajengea nyumba ili kuwapunguzia adha ya ukosefu wa makazi bora  na kuwafanya wawe na afya bora, furaha na amani.

Akizungumza na mtandao wa www.kasuludc.go.tz, diwani wa viti maalum kata ya Makere Bi. Mwasi Mchunga, amesema mpango huo waliuanza baada ya kuanzisha zoezi la kukagua kaya zisizo na vyoo ambapo walibaini asilimia kubwa ya kaya zenye hali duni kiuchumi ndizo zisizo na vyoo. Kupitia vikao vya kamati ya maendeleo ya kata, waliunda kamati iliyochunguza na kubaini uhitaji mkubwa wa msaada ili kuhakikisha wakazi hao wanapata mahitaji muhimu sambamba na uwepo wa vyoo.

Msaada  unaotolewa na wakazi hao ni ujenzi wa nyumba, vyoo bora, manunuzi ya vyombo vya ndani  na malazi  kwa makundi yenye uhitaji ikihusishwa  wazee wa jinsia zote, walemavu, wajane  wanawake wenye watoto ambao wametelekezwa na waume zao na kaya zilizo masikini.

Kupitia vikao vyake,  kamati  hiyo iliwashawishi na kuwahimiza  wananchi wote kuona umuhimu wa kuchangia fedha na nguvu ili kuhakikisha wenzao wasiojiweza wanapata nyumba, vyoo malazi na mahitaji mengine muhimu, jambo ambalo wananchi kwa kauli moja waliafiki na kuanza utekelezaji kupitia viongozi waliopo katika vitongoji vyao kwa awamu mbalimbali.

“Wananchi wanapochangishwa au kutakiwa kuchangia nguvu,  wamekuwa wakijisikia huru  huchangia bila kusita na haupo mgogoro wowote uliokwisha jitokeza kutokana na uendeshwaji wa zoezi hilo katani hapa”amesema bi.Mchunga.  

Amewahamasisha wanajamii wanaopenda maendeleo na kujali thamani ya utu wa wengine wilayani Kasulu na kwingineko kote nchini,  waweze kufika Makere kwa ajili ya kujifunza utaratibu huo na wakaufanyie kazi pale wanapoishi kwani jamii zenye uhitaji zipo nchi nzima.Mbali ya kuwa ni utaratimu kusaidiana, hata imani za dini  zetu zinatuhamasisha kufanya hivyo kwa wahitaji.

Amehitimisha kwa kusema kuwa, kwa sasa kata ya Makere wanaelekea kupunguza hali ya watu kutokuwa na vyoo bora kwani kaya nyingi zina vyoo bora na vya kisasa vyenye hadhi ya kutunza utu wa mtu pamoja na kudhibiti magonjwa ya mlipuko. Aidha ujenzi wa idadi ya vyumba katika nyumba hizo huendana na idadi ya watu waliopo katika kaya husika kuendana na mahitaji halisi pia  misaada mingine hutolewa kwa walengwa kuendana na kiwango cha fedha kinachokuwa kimekusanywa na ni utaratibu endelevu.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • KASULU DC YAANZISHA SHAMBA DARASA LA VIAZI LISHE KUKABILIANA NA UTAPIAMLO

    June 15, 2025
  • KUU KASULU YAKAGUA MIRADI YA MWENGE

    June 13, 2025
  • MATUMIZI YA ZANA ZA UFUNDISHAJI YATAJWA KUONGEZA UFANISI SHULENI

    June 11, 2025
  • WALIMU SHULE YA MSINGI KISUMA WATOA SHUKRANI KWA WADAU WALIOCHANGIA SARE NA VIFAA KWA WANAFUNZI

    June 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.