Na Mwandishi Wetu
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kimetaka ushirikishwaji wa jamiii na viongozi wa chama hicho ngazi ya kata ambazo miradi ya maendeleo inatekelezwa ili ukamilikaji wake uweze kuwa na tija zaidi kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa leo Alhamisi Septemba 5,2024 na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kasulu, Mbelwa Chidebwe wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya wilaya hiyo kukagua utekelelezaji wa ilani ya chama hicho kwenye miradi inayotekelezwa Halmshauri ya Wilaya ya Kasulu.
“Kimsingi tunaendelea na ziara kukagua utekelezaji wa ilani kwenye miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu…yapo maeneo tumepita ambayo ushirikishwaji wa viongozi wa chama na wananchi tumekuta miradi inaendelea vizuri,” amesema.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Mhe. Kanali Isaac Mwakisu amewataka wataalam hasa wale wanaohusika na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kubadilika ili waendane na utaratibu wa kisasa unavyoelekeza wa ufanyaji ukadiriaji wa vifaa ambao utakidhi matakwa ya maradi.
“Haiwezekani unajenga choo ukakadiria vitu kama unajenga ghorofa lazima ukadirie kama utaalam unavyotaka kufanya na wewe ni mzoefu tunategemea mazuri kutoka kwako kwakuwa umesoma katika fani hiyo…Mhe. Rais amekuwa anasisitiza sana jambo hili la miradi hivyo ni jukumu letu kama wataalam kuhakikisha tunaitekeleza katika ubora,” amesema.
Katika ziara hiyo kamati hiyo iletembelea ujenzi wa nyumba ya walimu ya mbili kwa moja katika Sule ya Sekondari Kamuganza,Matundu 13 ya vyoo Shule ya Msingi Kwiliba,madarasa matatu na vyoo vitano Shule ya Sekondari Nkundusi,Zahanati ya Chekenya na pia walifanya ukaguzi wa vifaa kwenye Kituo cha Afya cha Rungwe Mpya.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.