• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

UWEPO WA OFISI ZA NRFA WILAYANI KASULU UTASAIDIA WAKULIMA KUWA NA UHAKIKA WA SOKO

Posted on: May 5th, 2024

Na Mwandishi Wetu 

Kufunguliwa kwa ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NRFA) wilayani Kasulu  utatengeneza soko la uhakika la mazao utakaosaidia wakulima kujikomboa kiuchumi hivyo  pato la kaya kuimarika.

Katibu Tawala  wa Wilaya ya Kasulu, Theresia Mtewele ameyabainisha hayo jana  kwenye sherehe ya  siku ya wakulima wa zao la Mpunga zilizofanyika  katika Kijiji cha Titye wilayani humo.

“NRFA mwaka huu itaanza kununua mazao ikiwemo Mpunga tofauti na hapo awali soko lilipokuwa linaendeshwa na wafanyabiashara  tulipokea malalamiko katika masuala ya vipimo hivyo NRFA itazingatia uaminifu  wakulima wasiweze kuibiwa,” amesema.

Aidha, amebainisha kuwa serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji  pamoja na kuhimiza tafiti za mbegu bora zinazoweza kukabiliana na changamoto za kimazingira.

Katika hatua nyingine Theresia  amewapongeza wananchi wa kijiji hicho kwa  kuunganisha nguvu na kutengeneza  miundombinu ya madaraja  ambapo ametoa ahadi ya kuwasiliana na Wakala wa Barabara Vijiji na Mjini  (Tarura) kuifanyia maboresho.

Naye Mkurugenzi -TARI Kihinga, Dkt. Filson Kagimbo amesema  mradi wa urutubishaji wa mazao (NUT-CAT) unafanyika katika nchi kumi barani Afrika kwenye mazao ya Ngano, Mahindi, Mpunga na Teff.

“Kwa hapa Tanzania mradi huu unafanyika katika Mkoa wa Kigoma kwenye wilaya tatu za Kakonko, Kasulu na Kigoma …hapa Kasulu Mahindi tunafanya katika kata za Nyenge, Rusesa na Kwaga huku kwa zao la Mpunga tunafanya katika Skimu ya Umwagiliaji ya Titye,” amesema.

Amesema kupitia tathimini waliyoifanya wamejiridhisha kuwa  mavuno yameongezeka kutoka gunia tano hadi 12 ilivyokuwa awali na kufikia 25 mpaka 31 kwa heka moja.


Mhandisi wa Kilimo Mkoa wa Kigoma, Bathromeo Morice amesema kuwa  kutokana  na wakulima kufuata ushauri wa kitaalam  umesaidia mkoa kupata zawadi ya uzalishaji wa mazao ya Mahindi na Mpunga katika sherehe za Nanenane za mwaka uliopita mkoani Mbeya.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Kasulu, Everine Reuben  amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyowawezesha wakulima wa sekta ya umwagiliaji.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • KASULU DC YAANZISHA SHAMBA DARASA LA VIAZI LISHE KUKABILIANA NA UTAPIAMLO

    June 15, 2025
  • KUU KASULU YAKAGUA MIRADI YA MWENGE

    June 13, 2025
  • MATUMIZI YA ZANA ZA UFUNDISHAJI YATAJWA KUONGEZA UFANISI SHULENI

    June 11, 2025
  • WALIMU SHULE YA MSINGI KISUMA WATOA SHUKRANI KWA WADAU WALIOCHANGIA SARE NA VIFAA KWA WANAFUNZI

    June 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.