Na Mwandishi Wetu Kasulu
Kamati za huduma za mikopo ngazi ya kata zimetakiwa kufanya upembuzi yakinifu ili kuvipata vikundi sahihi vyenye uwezo wa kukopesheka na kufanya marejesho ya mikopo ya 10% inayotolewa na halmshauri kwakuwa mchakato mzima hadi kuvipata kupitia muongozo mpya unaanzia kwao.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kasulu, Emmanuel Ladislaus amebainisha hayo jana wilayani Kasulu mkoani Kigoma wakati wa Mafunzo ya Mikopo ya Wanawake,Vijana na Watu wenye Ulemavu kwa kamati hizo.
“Mikopo hii itakuwa na mchujo kuanzia ngazi ya chini na nyinyi mmeitwa kwasababu ndio shina kama katika ngazi yenu mtatoa taarifa za uongo basi kamati ya mikopo ya wilaya itafanyia kazi taarifa za uongo jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa taifa letu,” amesema.
Naye Mwenyekiti wa Mikopo ya 10% Halmshauri ya Wilaya ya Kasulu, Ndelekwa Vanica amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwapatia weledi washiriki ili kwenda kuhamsisha wananchi waunde vikundi ambavyo vitakuwa na sifa ya kukopesheka.
Mratibu wa Mikopo hiyo, Pelimina Msuta amesema kuwa kigezo kikubwa kitakachoangaliwa kwenye utoaji wa mikopo hiyo ni mwanakikundi mmojawapo kutokuwa na ajira rasmi kwakuwa mtu wa aina hiyo huwa na fursa ya kukopesheka katika taasisi mbalimbali za kifedha.
Katika hatua nyingine Mtendaji wa Kata ya Kalela, Hassan Makwepa amesema kuwa mafunzo hayo yamemsaidia kwenda kufanya hamasa kwa wananchi wenye nia ya kuchukua mikopo hiyo pamoja na kuvipatia ushauri sahihi kupitia maandiko yao ya biashara.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.