• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

"SHIRIKIANENI KATIKA UTENDAJI KUPATA MATOKEO MAKUBWA" DED KASULU

Posted on: January 7th, 2019

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mha. Godfrey Kasekenya (aliyesimama)akielezea jambo wakati wa ufunguzi mafunzo Elekezi kwa watumishi wa Idara ya Afya (hawapo pichani). Kulia kwake ni Afisa Utumishi Charles Millinga. (wa kwanza kushoto) Dk. Robert Rwebangira Kaimu Mganga Mkuu wilaya, akifuatiwa na Afisa Tawala  Ndg. Nicholaus  na watatu ni Katibu wa Afya  Ndg. Joseph Mwanambesi.

Watumishi wa Idara ya Afya wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kasulu(hayupo pichani) wakati wa Ufunguzi wa mafunzo Elekezi kwa watumishi walioajiriwa kuanzia Mwaka 2017, Waganga wakuu wa Vituo vya Afya na Zahanati yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Kasulu.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mhandisi Godfrey Kasekenya, amewataka wakuu wa vituo vya Afya na Zahanati kufanya kazi  kwa kushirikiana na watumishi walio chini yao ili kupata matokeo makubwa ya utendaji kazi ambayo ni tija kwa halmashauri na Taifa kwa ujumla.

Ameyasema hayo leo tarehe 7.1.2019 alipokuwa akifungua Mafunzo elekezi kwa Watumishi wa Idara ya Afya walioajiriwa kuanzia mwaka 2017, Waganga wakuu wa Zahanati na vituo vya Afya yaliyolenga kuwakumbusha Sheria na Maadili ya utumishi wa Umma, usimamizi wa fedha, na taratibu za kiutendaji kwa Kada ya Afya wilayani hapa.

“Ukiwa kiongozi wa Kituo cha Afya au Zahanati, ukaunda timu ya kufanya kazi na mkashirikiana vizuri na watumishi walio chini yenu kwa kuzingatia umoja, upendo,ushirikiano na mkafanya kazi kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa, lazima mtapata matokeo makubwa na mazuri” amesema Kasekenya.

Amewasisitiza watumishi hao kuhakikisha wanasimamia matumizi ya Fedha zinazoelekezwa vituoni kwa kuzingatia miongozo, kudhibiti upotevu wa dawa, kuweka ulinzi kwenye Zahanati  na vituo vya Afya, kujiendeleza kitaalumana na kutulia vituoni kwani maeneo mengi ya wilaya ya kasulu yanafikika na yana huduma nyingi muhimu.

Kaimu Mganga Mkuu Wilaya, Dk.Robert Rwebangira amesema Mafunzo na maelekezo  hayo yamelenga  kuwajengea uwezo watumishi hao katika utendaji kazi wenye  Weledi na kuwasaidia maelekezo na ushauri utakaowapa mwanga katika utatuzi wa changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo kiutendaji kazi.

“Pia kupitia mafunzo haya, watafahamu na kutekeleza dhana ya ugatuzi wa madaraka toka Halmashauri mpaka kwenye vituo vya Afya na Zahanati”amesisitiza Rwebangira.

Ndg. Joseph Mwanambesi  ambaye ni Katibu wa Afya Wilaya, amesema kuwa, kupitia mafunzo hayo anatarajia watumishi husika watatoa huduma bora kwa wananchi na kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni na taratibu za kiutumishi hali itakayoondoa migogoro isiyo ya lazima baina yao na waajiri hali kadhalika wananchi wanaowahudumia.

Upande wake Bi. Vailet Raymond ambaye ni Afisa Tabibu wa Kituo cha Afya Nyenge, amesema mafunzo hayo yamesababisha  atambue masuala mbalimbali ikiwemo Sheria za kiutumishi, miundo ya vyeo, taratibu  na kanuni za utendaji kazi.

“Binafsi niseme mafunzo haya yamenipa mwanga na kupelekea kujitambua nafasi yangu kama mtumishi wa Umma na ninajisikia kuanza utendaji kazi upya” amesisitiza Vaileth.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • KASULU DC YAANZISHA SHAMBA DARASA LA VIAZI LISHE KUKABILIANA NA UTAPIAMLO

    June 15, 2025
  • KUU KASULU YAKAGUA MIRADI YA MWENGE

    June 13, 2025
  • MATUMIZI YA ZANA ZA UFUNDISHAJI YATAJWA KUONGEZA UFANISI SHULENI

    June 11, 2025
  • WALIMU SHULE YA MSINGI KISUMA WATOA SHUKRANI KWA WADAU WALIOCHANGIA SARE NA VIFAA KWA WANAFUNZI

    June 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.