Na Mwandishi Wetu
Serikali imepongezwa kwa hatua iliyochukua ya kuruhusu watoto kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza hata kama baaadhi ya mambo muhimu ikiwemo vifaa vya shule hayajakamilika.
Pongezi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti leo Jumanne na baadhi ya wazazi waliowapeleka watoto wao kwenda kujiunga na elimu hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Mmoja ya wazazi, Stephano William kutoka Kijiji cha Nyangwa aliyempeleka mtoto wake kuanza masomo hayo katika Shule ya Sekondari Makere alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua aliyochukua ya kuhakikisha watoto wanafika shule hata kama hawajakamilisha vifaa vinavyotakiwa.
“Pongezi nayoitoa kwa serikali ni kwamba waendelee kutushika mkono kwenye upande wa elimu ili izidi kupamba moto tuondoe ujinga kwa watoto wetu ili siku za mbeleni waweze kutimiza ndoto zao,” amesema.
Naye Mengi Ndinagwe kutoka Kijiji cha Kitagata amesema kuwa alipofika katika shule ya Sekondari Kimwanya alikumbana na baadhi ya changamoto ambazo kwa muda mfupi ziliweza kutatuliwa.
“Na sasa wanaendelea kupokea wanafunzi ili mradi aje na daftari na kalamu hivyo ndivyo mzazi anatakiwa aje navyo ila suala la kupokelewa kwa hapa kwakweli hamna tatizo,” amebainisha.
Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Makere, Majid Jambia amesema kuwa wanaendela kupokea wanafunzi kupitia maelekezo waliyopewa kutoka ngazi za juu.
“Tunashukuru maafisa wetu kututembelea kwa hapa zoezi linaendelea vizuri na wamepata fursa ya kuongea na wanafunzi pamoja na wazazi, na zile changamoto zilizojitokeza ametusaidia pamoja kutupa maelekezo zaidi,” amesema.
Kwa upande wake Afisa Elimu Taaluma (Sekondari) Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Mussa Kanyoe amebainisha kuwa ametoa melekezo kwa shule zote kuwapokea watoto hata wale ambao hawana vifaaa ili ufundishaji utakapoanza waende sambamba.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.