• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

SERIKALI IMEONGEZA BAJETI KWENYE SEKTA YA KILIMO,MIFUGO NA UVUVI ILI KUIMARISHA UKUAJI WAKE

Posted on: August 9th, 2024

Na Mwandishi Wetu

Serikali imekuwa inaongeza bajeti kwenye Wizara ya Kilimo pamoja na ile ya Mifugo na Uvuvi ili kuimarisha masuala ya ugani na miundombinu ikiwa na lengo la kuwezesha ukuaji wa sekta hizo muhimu zinazogusa maisha ya watanzania wengi.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paulo Chacha amebainisha hayo jana wakati akifunga maonesho ya Nanenane Kanda ya Magharibi yaliyokuwa yanaendelea mkoani humo.

Amesema kupitia ongezeko hilo la bajeti serikali iliandaa Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ili kuwavutia vijana kuwekeza katika sekta ya kilimo,mifugo na uvuvi na kuhakikisha soko linakuwepo kwa  kile kitakachozalishwa.

“Kupitia BBT serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuwawezesha vijana kujenga kesho iliyo bora kwa kuwapa mafunzo ya kufanya kilimo kilicho bora kupitia mikakati mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu na mbinu mbalimbali za kufanya kilimo na ufugaji wenye tija,” amebainisha.

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Mhe. Kanali Michael Ngayalina aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mhe. Thobias Andengenye amesema kuwa umuhimu wa sekta ya mifugo na ufugaji unajieleza wazi kwakuwa ni nyenzo muhimu kwenye kujitosheleza kwa chakula hivyo uzalishaji wake kuwa na uhakika wa soko.

Na kuongeza kuwa juhudi za dhati zinatakiwa kufanywa kwenye sekta za kilimo,mifugo na uvuvi ili kusaidia uzalishaji wa kutosha wa malighafi kwa ajili ya uchakataji viwandani kitu kitakachosaidia kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao yanayotokana na sekta hizo.

Naye Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo, Eliasifu Mlai aliwahimiza wakulima kutumia teknolojia sahihi katika kilimo wanachokifanya ikiwemo matumizi ya mbegu bora ili  kiwango cha uzalishaji wa mazao kipate kuongezeka.  

Katika hatua nyingine Mwakilishi wa Wakulima, Wafugaji na Wavuvi Kanda ya Magharibi,Mathias Zacharia amewataka wakulima kujiunga na Bima ya Mazao ili wawe na uhakika wa usalama wa kile wanachokizalisha mashambani.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • KASULU DC YAANZISHA SHAMBA DARASA LA VIAZI LISHE KUKABILIANA NA UTAPIAMLO

    June 15, 2025
  • KUU KASULU YAKAGUA MIRADI YA MWENGE

    June 13, 2025
  • MATUMIZI YA ZANA ZA UFUNDISHAJI YATAJWA KUONGEZA UFANISI SHULENI

    June 11, 2025
  • WALIMU SHULE YA MSINGI KISUMA WATOA SHUKRANI KWA WADAU WALIOCHANGIA SARE NA VIFAA KWA WANAFUNZI

    June 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.