Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Madiwani, Wataalam pamoja na waalikwa wakimsikiliza Diwani wa Kata ya Kagerankanda Mhe. Ezekiel Mshingo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu kitalu cha uwindishaji wa Kkitalii cha Makere-Uvinza Open Area kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma(Hayupo pichani)
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu. Emmanuel Maganga akisisitiza jambo mara baada ya kupokea taarifa ya Eneo la kitalu cha uwindishaji wa kitalii cha Makere-Uvinza Open Area Kasulu.
Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Madiwani, Wataalam pamoja na waalikwa wakisilkiliza maelekezo na ushauri kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu leo Tarehe 16.09.2019
Na. Andrerw Ginnethon-Kasulu.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga, amefanya kikao kazi na Braza la Madiwani pamoja na Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu na kusisitiza utendaji kazi unaozingatia uadilifu na kusimamia utekelezaji wa maazimio wanayokubaliana kwenye vikao vya kisheria ili kuepuka migogoro inayopelekea kushindwa kusimamia kitalu cha uwindishaji kilichopo wilayani hapa.
Magaga ameyasema hayo leo tarehe 16,9,2019 baada ya kupokea taarifa ya Eneo la Kitalu cha uwindishaji wa kitaalii cha Makere Fr-Uvinza Open Area kisha kujadili changamoto zinazotokana na shughuli mbalimbali za kibinaadamu ambazo haziendani na uhifadhi wa wanyamapori na matakwa ya Ardhi Oevu zinazoathiri kitalu hicho.
Akipokea mawazo na ushauri kutoka kwa Wah. Madiwani kuhusu kukabiliana na changamoto hizo, Mkuu wa Mkoa amewaasa kuwa waadilifu na kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu, kanuni na Sheria wakilenga maslahi ya Nchi.
“Utendaji kazi wenye uadilifu na uaminifu pia kusimamia kile tunachokubaliana kwenye vikao, utaepusha migogoro isiyo ya lazima inayosababishwa na uwepo wa maamuzi tofauti kwa baadhi yenu hali itakayopelekea kutofikiwa kwa malengo katika mipango ya Halmashauri” Amesisitiza Maganga.
Akitoa taarifa fupi ya Kitalu hicho, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kan. Simon Anange, amesema Wah. Madiwani wahakikishe wanawasaidia wataalam katika kusimamia utekelezaji wa maazimio wanayopanga ili kuepuka mikwamo ya kiutendaji katika usimamizi na uendelezaji wa Kitalu.
“Madiwani simamieni kwa ukamilifu utekelezaji wa maazimio yenu ikiwemo ulinzi na uendelezaji wa Kitalu chetu na tushirikiane kutatua changamoto zote zinazojitokeza kwa manufaa ya Halmashauri ya Kasulu na siyo kundi la watu au mtu binafsi” amesisistiza Kan. Anange.
Akisoma taarifa ya Eneo la kitalu cha uwindaji wa kitalii, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema Mwaka 1996 Wizara ya Maliasili na Utalii iliridhia ombi kuhusu kutambua rasmi eneo wazi lenye ukubwa wa Kilomita za mraba elfu mbili miatano tisini na moja kuwa kitalu cha uwindishaji kwa jina la Makere Forest Reserve/Uvinza Open Area.
Kupitia taarifa hiyo, Mkurugenzi amefafanua kuwa lengo la Halmashauri katika uidhinishaji wa kitalu hicho ni uhifadhi wa bioanuai, Ardhi oevu katika Mto Malagarasi, wanyama pori, misitu na Kuongeza mapato ya Halmashauri.
Aidha Kasekenya amefafanua kuwa, mpaka sasa kitalu hicho kipo chini ya Kampuni ya Wengert Windrose Safari Ltd inayoendesha shughuli za uwindaji wa kitalii na uhifadhi. Kampuni hiyo imeweka miundombinu mbalimbali ikiwemo uwanja wa ndege, Barabara, Kambi zenye mahema, mnara wa mawasiliano pamoja na boti kwa ajili ya watalii na ufanyaji wa Doria.
Amezitaja changamoto zinazokabili eneo la kitalu ikiwa ni ongezeko la shughuli za kibinaadamu kama makazi, kilimo, ufugaji , uwindaji haramu (ujangili), na ugawaji holela wa Ardhi unaofanywa na kundi la wananchi wasiotii Sheria na kuzingatia kanuni na taratibu za Nchi.
Kasekenya amehitimisha kwa kufafanua kuwa, pamoja na uwepo wa changamoto hizo ni muhimu kitalu kiendelee kulindwa kwa kuwaondoa wavamizi na wananchi wengine waliofanya makazi katika eneo la Ardhi oevu.
‘’Mwekezaji anashindwa kuwekeza kwa nguvu kutokana ukosefu wa usalama eneo la kitalu na uvamizi unaoendelea kwa baadhi ya wavamizi kuua wanyama kwa kutumia sumu, kuingiza mbwa katika hifadhi na mifugo inayosababisha uharibifu mkubwa wa mazingira” amehitimisha Kasekenya.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.