• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

NZUNDA AKAGUA UJENZI WA KITUO CHA BIASHARA MJINI KASULU.

Posted on: November 12th, 2018

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kasulu Mhandisi Godfrey Kasekenya akifafanua jambo mara baada ya kuwasilisha taarifa ya ujenzi wa Kituo cha biashara mjini Kasulu. Kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Ndg. Rashid Mchanga na wa tatu kushoto ni Naibu katibu Mkuu ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Bw. Tixon Tuliangine Nzunda.

Naibu katibu Mkuu ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu  Bw. Tixon Tuliangine Nzunda akikagua maendeleo ya ujenzi wa       miundombinu ya kuhifadhia maji taka katika Jengo linalokamilishwa la Kituo cha Biashara kilichopo Mjini Kasulu.

Jengo la kituo cha Biashara “One Stop Business Centre lililopo Mjini Kasulu.


Na. Andrew Mlama-Kasulu.

Naibu katibu Mkuu ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu  Bw. Tixon Tuliangine Nzunda amekagua na kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Biashara cha Wilaya “One Stop Business Centre” kilichopo kata ya Kimobwa Mjini Kasulu.

Nzunda amekagua kituo  hicho leo tarehe 12.11.2018 akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa kuboresha Mazingira ya Biashara(Local Investment Climate-LIC) mkoani Kigoma. Mradi huo wa kituo cha Biashara “One Stop Business Centre” umetekelezwa na LIC ikishirikiana na Halmashauri ya mji na wilaya  ya Kasulu ambapo umegharimu  shilingi. 49,977,177.61.

Amesisitiza  watendaji kuhakikisha wanatekeleza maelekezo yote wanayoyapata ili kufikia malengo yaliyowekwa na yanayoendelea kuwekwa na Serikali. Aidha amesema,  hatoweza kumfumbia macho mtu yeyote atakayebainika kuzorotesha shughuli za maendeleo kwa namna yoyote.

“Nimeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa kituo hiki na ninakuagiza Mkuu wa Wilaya uhakikishe kinafunguliwa na kuanza kutumikahivi karibuni” amesema  Nzunda baada kumaliza  kukagua Kituo hicho.

Akiwasilisha taarifa  ya miradi iliyotekelezwa na inayotegemewa kutekelezwa na LIC, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kasulu Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema mpaka sasa kituo kipo kwenye hatua za mwisho za ujenzi na mafundi wanakamilisha mfumo wa maji safi na maji taka pamoja na kuunganisha Umeme.

Amesema wanaotarajiwa kutoa huduma katika jengo hilo ni pamoja na maafisa biashara wa halmashauri za mji na wilaya ya Kasulu, Afisa toka mamlaka ya mapato, huduma za kibenki, TCCIA pamoja na BRELA.

Amefafanua kuwa, mpaka sasa vimeshapokelewa vifaa mbalimbali kutoka LIC ambavyo ni Kompyuta sita, Printa moja, meza sita, Kabati sita,Viti vya Ofisini kumi na nane pamoja na viti sita vya wageni.

“Tunatarajia kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wateja wetu na kuimarisha mahusiano na taasisi mbalimbali” amehitimisha Kasekenya.

Nzunda ameendelea na ziara yake ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa na Mradi wa kuboresha mazingira ya biashara (LIC) mkoani hapa.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • KASULU DC YAANZISHA SHAMBA DARASA LA VIAZI LISHE KUKABILIANA NA UTAPIAMLO

    June 15, 2025
  • KUU KASULU YAKAGUA MIRADI YA MWENGE

    June 13, 2025
  • MATUMIZI YA ZANA ZA UFUNDISHAJI YATAJWA KUONGEZA UFANISI SHULENI

    June 11, 2025
  • WALIMU SHULE YA MSINGI KISUMA WATOA SHUKRANI KWA WADAU WALIOCHANGIA SARE NA VIFAA KWA WANAFUNZI

    June 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.