Na Mwandishi Wetu,Kasulu
Kijiji cha Buhoro leo Ijumaa Desemba 6,2024 kimeupokea mradi wa Wezesha Binti uliotambulishwa na Shirika la Maendeleo la Ubelgiji (ENABEL) wenye lengo la kuwakwamua vijana wenye umri wa miaka 14-29 wanaoishi katika mazingira magumu.
Akizungumza wakati wa tukio hilo Diwani wa Kata ya Buhoro,Mathias Sunzu ameipongeza ENABEL kwa namna Ilivyolenga kuwapa ujuzi vijana wa jinisa zote kufanya kazi mchanganyiko pamoja na kumfanya mtoto wa kike kuwa na hedhi salama akiwa shuleni.
“Mradi huu utatekelezwa katika Shule ya Sekondari ya Ntamya na wananchi wamehamasika kuunga mkono kama unavyoona kwakuwa umeweka kipaumbele kutoa taulo za kike pamoja na kujenga vyoo vya kisasa vyenye uhakika wa maji ili viwasaidie wakati wa hedhi,” amesema.
Pamoja na hayo ameiomba ENABEL kuiwezesha shule hiyo ujenzi wa mabweni mawili ya watoto wakike na moja wakiume ili kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilomita 12 kufika shuleni.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Wezesha Binti, Henry Abraham amesema kuwa wamebaini jamii ina changamoto nyingi zinazohitaji utatuzi hivyo wakianza rasmi kutekeleza mradi huo kijijini hapo watahakikisha wanazitatua ili idadi ya wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne iweze kuongezeka.
Katika hatua nyingine Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Ntamya,Welason Said amesema kuwa majadiliano yaliyofanyika yamempa weledi wa kuwasaidia watoto wa kike wanapopitia changamoto mbalimbali wakati wa hedhi ikiwemo kuripoti vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa kwa mamlaka husika.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.