Naibu katibu mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Amon Mpanju (mwenye fimbo nyeupe) akiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa halmashauri Yohana Mshita na kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kasulu Mhandisi Godfrey Kasekenya.
Na.Andrew Mlama. Kasulu
Naibu katibu mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Amon Mpanju, amefungua warsha ya siku mbili kwa wadau wa wa Kampeni ya ulinzi wa wanawake na watoto dhidi ya ukatili wanaotendewa na baadhi ya wanajamii.
Kabla ya kukutana na wadau hao, Ndg Mpanju aliongea na Wah. Madiwani wa wilaya ya Kasulu leo tarehe 17/09/2018, ambapo aliwasisitiza, kama viongozi waone umuhimu wa kusimamia na kudhibiti kisheria tabia za jamii kutekeleza ukatili dhidi ya mwanamke na mtoto.
Akizungumza na wadau wa ulinzi wa wanawake na watoto katika ukumbi wa chuo cha ualimu Kasulu, amesema kuwa taasisi za serikali, dini na wadau wengine waone umuhimu wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii kwani huathiri amani na utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
“Kiwango kikubwa cha watoto huacha shule huku takwimu zikionyesha asilimia 47 ya wanafunzi wa shule za msingi na asilimia 40 wa sekondari, wameacha shule kati ya mwaka 2017 hadi 2017 kutokana na vitendo vya ukatili dhidi yao” amesema Mpanju.
Mmoja wa wadau wa ulinzi wa wanawake na watoto ndg Almachius Njungani, amesema kuwa kuna faida kubwa kwa jamii kutambua umuhimu wa kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwani hudhalilisha utu pamoja na kuchelewesha maendeleo ya kielimu na kiuchumi.
“Elimu inahitajika sana katika jamii ili kutambua madhara yatokanayo na ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii yetu” alihitimisha Njungani.
Warsha hiyo imelenga kuwajengea uwezo washiriki juu ya masuala ya kisheria kwa lengo la ulinzi wa wanawake na watoto wilayani hapa.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.