• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

KIKAO CHA WADAU WA ELIMU CHAJADILI NAMNA YA KUPAISHA UFAULU

Posted on: February 6th, 2025

Na Mwandishi Wetu,Kasulu

Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kupitia Idara ya Elimu Msingi imefanya kikao cha wadau wa elimu wa Kata ya Mvugwe na Makere kwa ajili ya kuweka mikakati ya ufaulu wa mitihani ya darasa la nne na darasa la saba kwa mwaka wa masomo 2025.

Kikao hicho kilichofanyika  hivi karibuni katika Shule ya Msingi Mvugwe kilihusisha wenyeviti wa kamati za shule,viongozi wa dini,viongozi wa serikali za vijiji,walimu,polisi kata,wazee maarufu na watu wa taaluma kutoka makao makuu ya halmashauri.

Akizungumza katika kikao hicho Mratibu wa Timu ya Ufuatiliaji, Respice Swetu amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kupata tathimini kwa ngazi ya kata ni mikakati ipi iwekwe ili kuongeza kiwango cha ufaulu.

“Hapa tunaangalia ni kitu gani kinatakiwa kufanywa kwakuwa mwaka uliopita tulikuwa wa kwanza kimkoa katika mitihani ya darasa la nne na wa pili kimkoa katika mtihani wa darasa la saba tukaona walimu ndio hasa waliotekeleza kazi hiyo wakishirikiana na wadau hivyo tupo hapa kushirikishana yanayotakiwa kufanyika ili mafanikio hayo tuliyopata yaimarike zaidi,” amesema.

 Kwa upande wake Afisa Elimu Taaluma wa Halmashauri hiyo,  Joseph Maiga amesema kuwa  utekelezaji wa mikakati iliyowekwa ili iweze kuwa na mashiko ni lazima walimu wabaini kiwango cha uelewa baina ya wanafunzi ili waweze kwenda nao wote sambamba.

Mmoja wa washiriki wa kikao hicho,Mkebyela Elias amesema kuwa mikakati iwekwe ili suala la chakula liwe kwa madarasa yote na si tu yale ya mitihani kitu kitakachosaidia watoto kupenda shule na ufaulu kuongezeka.


Akifunga mkutano huo Diwani wa Kata ya Mvugwe, Mhe. Nuhu Abel amewataka wazazi kuacha dhana potofu ya kuwa chakula wananchochangia shuleni kinaenda kuwanufaisha walimu kitu kinachosababisha mara nyingi zoezi hilo kuzorota.


Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • KASULU DC YAANZISHA SHAMBA DARASA LA VIAZI LISHE KUKABILIANA NA UTAPIAMLO

    June 15, 2025
  • KUU KASULU YAKAGUA MIRADI YA MWENGE

    June 13, 2025
  • MATUMIZI YA ZANA ZA UFUNDISHAJI YATAJWA KUONGEZA UFANISI SHULENI

    June 11, 2025
  • WALIMU SHULE YA MSINGI KISUMA WATOA SHUKRANI KWA WADAU WALIOCHANGIA SARE NA VIFAA KWA WANAFUNZI

    June 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.