Na Mwandishi Wetu
Wananchi mkoani Kigoma wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao wakati wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotarajiwa kuzinduliwa mkoni humo Julai 1,2024.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,Mhe. Jaji Jacobs Mwambegele wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ujiji siku ya jana Juni 19,2024.
Ambapo amewapongeza wadau wa uchaguzi mkoani humo kwa kuteuliwa kuwa sehemu ya uzinduzi wa uboreshaji wa daftari hilo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Kawawa uliopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.
"Uboreshaji wa daftari utazinduliwa hapa mkoani Kigoma Julai 1,2024 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa. Tayari tume imeamua kwamba uzinduzi huo utafanyika katika Uwanja wa Kawawa uliopo hapa kwenye Halmshauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji," amesema.
Amesema uzinduzi huo utatanguliwa na shughuli mbalimbali za uhamasishaji na tamasha la uboreshaji wa daftari ambalo litafanyika Juni 28,2024 katika uwanja huo.
Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi wa tume hiyo,Ramadhani Kailima amesema kuwa uboreshaji katika awamu ya kwanza utafanyika katika mizunguko 13 na mikoa itakayofuata baada ya Kigoma ni Katavi na Tabora.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.