• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

KASULU DC YATAKIWA KUSIMAMIA VIZURI WATENDAJI WA VIJIJI KWENYE UANDIKISHAJI UGAWAJI WA VYANDARUA VYA BURE

Posted on: March 13th, 2025

Na Mwandishi Wetu 

Ili kukabiliana na ugonjwa wa Malaria Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imetakiwa kuwasimamia vizuri watendaji wa kata na vijiji kwenye zoezi la uandikishaji wa kaya zinazotakiwa kupatiwa vyandarua kwakuwa  kutakuwa hakuna vile vya ziada kwa zile ambazo taarifa zao hazitachukuliwa.

Mwakilishi wa Wizara ya Afya-Mpango wa Kudhibiti Malaria (NMCP), Peter Gitanya amebainisha hayo jana kwenye Mkutano wa Uraghibishaji kwa viongozi wa halmshauri hiyo la zoezi la ugawaji wa vyandarua kwa ngazi ya kaya bila malipo.

“Uandikishaji huu utatumia njia ya simu hivyo hakikisheni viongozi wa vijiji hawateuwi mwandikishaji kutoka kijiji kingine na hakutakuwa na chandarua chochote cha ziada kwa kaya ambayo haijajiandikisha kwahiyo ukitokea upungufu ni mtendaji wa kijiji kakaa chini na waandikishaji wake kaamua kutudanganya,” amesema.

Pia, amesema kuwa halmashauri itakuwa na jukumu la kuhakikisha usalama wa vyandarua wakati wa usafirishaji wake pamoja na kusimamia matumizi ya rasilimali fedha kama ilivyokusudiwa.

Naye Mwakilishi wa Mratibu wa Malaria OR- TAMISEMI,January Bonventure amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2025-2026 serikali imesisitiza upangaji wa bajeti katika halmashauri hiyo uelekeze nguvu nyingi katika kukabiliana na ugonjwa  huo ili kusaidia unyunyiziaji wa dawa kwenye mazalia ya Mbu.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Komesha Kaminyoge amebainisha kuwa watahakikisha wanahamasisha wananchi   kujiandikisha katika kaya zao  ili wote waweze kupata vyandarua kwa kutumia vyombo vya habari,matangazo kwenye masoko ya jioni,viongozi wa dini na watu maarufu.

Katika hatua nyingine Mratibu wa Malaria  Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Dkt. Berlino Mlange amesema kuwa ugawaji wa vyandarua hivyo  ni agizo la utekezaji wa afua za malaria kwa ngazi ya taifa ndio maana halmashauri kwa makadirio ya awali inategemea kugawa vyandarua  vipatavyo 307,709.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • KASULU DC YAANZISHA SHAMBA DARASA LA VIAZI LISHE KUKABILIANA NA UTAPIAMLO

    June 15, 2025
  • KUU KASULU YAKAGUA MIRADI YA MWENGE

    June 13, 2025
  • MATUMIZI YA ZANA ZA UFUNDISHAJI YATAJWA KUONGEZA UFANISI SHULENI

    June 11, 2025
  • WALIMU SHULE YA MSINGI KISUMA WATOA SHUKRANI KWA WADAU WALIOCHANGIA SARE NA VIFAA KWA WANAFUNZI

    June 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.