• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

KASULU DC YAONYESHA USIMAMIZI MADHUBUTI WA MAPATO YA NDANI

Posted on: January 25th, 2023


HALMASHAURI Ya Wilaya Ya Kasulu imeonyesha kuwezekana kabisa kubadilisha changamoto kuwa fursa kwa kufanya kazi kubwa kupitia ukusanyaji wa pesa ndogo zitokanazo na mapato ya ndani endapo viongozi wa serikali watakuwa na uchungu katika usimamizi wa kutosha wa mapato hayo na dhamira ya dhati.

Aliyasema Hayo Mkuu Wa Mkoa Wa Kigoma Mhe. CGF (Rtd) Thobias Emir Andengenye alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika ufunguzi wa nyumba tano za kuishi watumishi wa Afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mnamo tarehe 26/01/2023.

Aidha alimpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia serikali anayoiongoza  kwa kuweka sheria ya kutenga 40% ya mapato ya ndani kwaajili ya kufanyia shughuli zinazoonekana na kuimarisha huduma ambazo zinawagusa wananchi wote kama hospitali, shule na maji.

"Nichukue nafasi hii kuushukuru sana uongozi wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Kasulu kwa mradi huu ambao kwanza ni maelekezo ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan lakini pili kwa kutumia pesa kidogo waliyonayo wametuonesha kumbe ukiwepo na usimamizi wa kutosha,kukiwepo na dhamira ya dhati, kukiwepo na uchungu kwa upande wa viongozi wa serikali inawezekana kabisa pesa kidogo zinazokusanywa kufanya kazi kubwa na kubadilisha changamoto kuwa fursa", alisema Mhe. andengenye 

Mhe. Andengenye aliwasihi  wananchi wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Kasulu kuendelee kutoa ada, ushuru na tozo mbalimbali bila kukwepa kwani matunda yake yanaonekana kupitia ukamilishaji wa miradi na kuleta maendeleo yanayonufaisha jamii husika kwa ujumla 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Kanali Issac Anthony Mwakisu aliwaomba wananchi wa Wilaya ya Kasulu kuendelea kuvumiliana na kufanya kazi kwa umoja kwa kuwa kazi moja walionayo ni kuhakikisha Kasulu inakwenda mbele na hakuna kiongozi alie na nia ya kuonea mtu bali kazi inafanyika kwa kufata maelekezo ya Serikali na kwaajili ya maslahi mapana ya nchi ya Tanzania.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa nyumba tano za Watumishi wa hospitali Mganga Mkuu Wa Hospitali Ya Halmashauri Ya Wilaya Ya Kasulu Dkt.Robert Nelson Rwebangira alisema Halmashauri hiyo inaendelea kupanua wigo wa huduma za afya kwa kujenga na kuboresha miundombinu ya afya kwa lengo la kufikia maendeleo endelevu hasa Afya na hali bora kwa wananchi wote ifikapo 2030

Mradi wa nyumba tano umegharimu jumla ya shilingi 291,551,400 hadi kukamilika sawa na shilingi 58,310,280 kwa kila nyumba kwa awamu ya kwanza katika wamu ya pili ya ujenzi wa nyumba nne zenye uwezo wa kuhifadhi familia tatu, unatarajiwa kugharimu jumla ya shilingi 535,373,852 sawa na shilingi 133,843,463 kwa kila nyumba ambapo inatarajiwa mradi utakapo kamilika kuhifadhi familia  17 za watumishi wa afya



Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • KASULU DC YAANZISHA SHAMBA DARASA LA VIAZI LISHE KUKABILIANA NA UTAPIAMLO

    June 15, 2025
  • KUU KASULU YAKAGUA MIRADI YA MWENGE

    June 13, 2025
  • MATUMIZI YA ZANA ZA UFUNDISHAJI YATAJWA KUONGEZA UFANISI SHULENI

    June 11, 2025
  • WALIMU SHULE YA MSINGI KISUMA WATOA SHUKRANI KWA WADAU WALIOCHANGIA SARE NA VIFAA KWA WANAFUNZI

    June 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.