Na Mwandishi Wetu,Kasulu
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kasulu imeipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kwa namna ilivyowashirikisha wananchi na wajumbe wa chama hicho katika kata ya Nyakitonto kwenye ujenzi wa shule mpya ya sekondari Luhunga.
Ushirikishwaji wa makundi hayo kwenye ujenzi wa shule hiyo uliotekelezwa kupitia fedha kutoka serikali kuu kiasi cha shilingi 603,890,563 umesaidia kwa kiasi kikubwa mradi huo kutekelezwa katika viwango vinavyotakiwa.
Akizungumza shuleni hapo wakati wa ziara ya kamati hiyo kwenye ukaguzi wa miradi kuangalia utekelezaji wa ilani ya chama hicho Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo, Mbelwa Chidebwe amesema kuwa ushirikishwaji wa makundi hayo umeondoa sintofahamu linapokuja suala zima la ukaguzi wa miradi.
“Niwapongeze hasa kwenye suala zima la ushirikishwaji watu wakifanya vizuri sisi kama chama chenye serikali tunaona raha tunapoenda kueleza hiki kwa wananchi tunakuwa hatutumii nguvu kubwa,” amesema Chidebwe.
Naye Katibu wa chama hicho Kata ya Nyakitonto,Shemu Kibiliti amesema kuwa ushirikishwaji wao wa 100% umewapa faraja kubwa kwa kuona wanathaminiwa hasa kwenye suala zima la usimamizi wa miradi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo, Ndelekwa Vanica amesema kuwa wataendelea kushirikiana na wadau wote kwenye suala zima la usimamizi wa miradi ili marekebisho na mapungufu yanayojitokeza yaweze kufanyiwa kazi.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.