Na Mwandishi Wetu
Katika kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan lililotaka kila mkoa kuhakikisha wilaya inafanya shughuli za kijamii kama njia mojawapo ya kusheherekea maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Dkt. Semistatus H. Mashimba ameongoza zoezi usafi katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu na vituo vyote vinavyotoa huduma za afya lililoambatana na uchangiaji wa damu kwa kushirikiana na Kambi ya Jeshi ya 825 JKT Mtabila.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi, Afisa Usafi na Udhibiti wa Taka wa Halmashauri hiyo , Ndelekwa Vanica amehimiza jamii kushiriki mazoezi hasa yale ya usafi ya kitaifa likiwemo lile la kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ili kusaidia mazingira kuwa katika hali ya usafi.
“Serikali imeshatoa tamko kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ni wajibu wa kila mwananchi kushiriki shughuli za usafi na niwaombe kambi ya Mtabila kila tutakapowaita katika mazoezi hayo mje kama njia mojawapo ya kuhamasisha jamii kushiriki usafi huo,” amesema.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mageni Pondamali ameishukuru Kambi ya JKT Mtabila kwa uchangiaji wao wa damu kutokana na hospitali hiyo kuwa na uhaba wa huduma hiyo kitu kitakachosaidia kuokoa maisha ya watu wengi.
Katika hatua nyingine Mratibu wa Huduma za Maabara wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Jasimen Meru amesema kuwa zoezi la uchangiaji damu limesaidia ukusanywaji wa chupa 36 zenye ujazo wa 'Mils' 450 kwa kila moja zitakazokwenda kusaidia watu wenye matatizo ya Seli Mundu,wamama wajawazito,watoto chini ya miaka mitano pamoja na majeruhi wa ajali.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.