• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

Dkt.Mashimba akaribishwa Kasulu DC

Posted on: March 26th, 2024

Na Mwandishi Wetu


 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Mhe. Eliya Kagoma leo Jumanne  ameongoza kikao cha Baraza  la madiwani lililojikita kuwasilisha taarifa ya utendaji kazi  kwa ngazi ya kata katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2023/2024.

Ambapo madiwani, watumishi na wananchi walioudhuria kikao hicho walipata fursa ya kumkaribisha  Mkurugenzi mpya wa halmashauri hiyo, Dkt. Semistatus H. Mashimba .

Akitoa salamu za ukaribisho Kagoma amebainisha kuwa baraza hilo linaishi kama familia kwa kila mjumbe kutoa mawazo yake pasipo kubaguliwa kama anatoka chama tawala au upinzani.

“Karibu sana Kasulu sisi Baraza la Madiwani tunaishi kama familia tuna kata 14 zinazoongozwa na chama tawala, kata 7 zilizo chini ya wapinzani, viti maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) watano na  viti maalumu wawili kutoka upinzani,” amesema.

Na kuongeza kuwa : “Lakini hapa huwezi kujua CCM ni nani na mpinzani ni nani sisi tunaishi hivyo na kama kuna jambo Mwenyekiti anatakiwa kushauriwa napokea ushauri kutoka kona zote,”.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Dkt. Semistatus H. Mashimba alihaidi kulipa ushirikiano wa kutosha baraza  hilo na kutaka wamtumie vizuri katika kutatua changamoto zao mbalimbali.

“Niseme mbele ya baraza lako Mwenyekiti najikabidhi kwenu nikiondoka vibaya ni nyinyi na nikiondoka vizuri ni nyinyi hivyo mnilee kuna mambo nimetoka nayo huko nilipotoka mna wajibu wa kuniweka katika mstari,”.

Naye Diwani wa Kata ya Asante Nyerere, Mhe. Julius Mpwehuka amesma kuwa kata yake imefanikiwa katika suala la chakula la mashuleni baada ya kuwaelimisha wazazi umuhimu wa kushirikiana na serikali katika kufanikisha jambo hilo.

Katika hatua nyingine Diwani wa Kata ya Nyamnyusi aliishukuru serikali kwa namna inavyotatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi kwa kujenga shule, vituo vya afya na zahanati pamoja na kurejesha ruzuku ya mbolea kwa wananchi.





Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • KASULU DC YAANZISHA SHAMBA DARASA LA VIAZI LISHE KUKABILIANA NA UTAPIAMLO

    June 15, 2025
  • KUU KASULU YAKAGUA MIRADI YA MWENGE

    June 13, 2025
  • MATUMIZI YA ZANA ZA UFUNDISHAJI YATAJWA KUONGEZA UFANISI SHULENI

    June 11, 2025
  • WALIMU SHULE YA MSINGI KISUMA WATOA SHUKRANI KWA WADAU WALIOCHANGIA SARE NA VIFAA KWA WANAFUNZI

    June 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.