Na Mwandishi Wetu,Kasulu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu,Dkt. Semistatus H. Mashimba leo Ijumaa amekutana na kufanya kikao na viongozi na wachezaji wa timu ya Nyakitonto FC.
Ambapo kupitia kikao hicho ameuelekeza uongozi wa timu hiyo pamoja na Kitengo cha Michezo cha Halmashauri wakae kwa pamoja kuona ni namna gani wanaweza kubadilisha jina na kuwa Kasulu DC FC.
"Niwaombe viongozi wa timu mkae pamoja na Kitengo cha Michezo kuona ni jinsi gani mtabadilisha jina la timu ili iweze kuendeshwa kisasa na kuboreshewa miundombinu ya mazoezi kupitia udhamini wa halmashauri," amesema.
Aidha,Dkt. Mashimba amesisitiza ili kuweka motisha kwa wachezaji kuweza kufanya vizuri halmashuri itahakikisha inawaingiza katika malipo ya kila mwezi pamoja na posho mbalimbali za kujikimu.
Katika hatua nyingine amemtaka Afisa Michezo kwenda kujifunza katika halmashauri zingine zinazomiliki timu ni namna gani zimeweza kufanikiwa katika nyanja hiyo.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.