• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

DED KASULU AFUNGUA MRADI WA UJENZI WA MADARASA NA OFISI YA WALIMU S. M.NYAKASANDA.

Posted on: November 21st, 2018

Jengo la madarasa  mawili na Ofisi ya Mwalimu Mkuu katika shule ya Msingi Nyakasanda lililofunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kasulu, Mhandisi Godfrey Kasekenya leo tarehe 21.11.2018 katani Nyachenda.

Mkurugenzi wa Hmalmashauri ya Kasulu, Mha. Kasekenya (mwenye suti Nyeusi) akielekea kufungua mradi wa ujenzi wa madarasa na ofisi ya Mwalimu Mkuu katika shule ya Msingi Nyakasanda. Kushoto kwake ni Mratibu Elimu wa Kata ya Nyachenda Ngd. Jonas Donge.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kasulu Mha. Godfrey Kasekenya (wa kwanza kulia) akiwa katika Picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Halmashauri pamoja  na Kata ya Nyachenda mara baada ya kukata Utepe  kuashiria ufunguzi rasmi wa majengo mawili ya madarasa pamoja na Ofisi katika Shule ya msingi Nyakasanda.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza wakati wa ufunguzi wa madarasa na Ofisi katika shule ya msingi nyakasanda, wakisikiliza hotuba  ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kasulu mara baada ya ufunguzi wa jengo la Madarasa na Ofisi katani Nyachenda.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Kasulu, Mha. Kasekenya (aliye kaa katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kijiji, kata na halmashauri, mara baada ya kukagua Ofisi ya Mwalimu Mkuu aliyoifungua pamoja na madarasa mawili katika shule ya msingi Nyakasanda iliyopo kwenye Kata ya Nyachenda wilayani hapa.

Na. Andrew Mlama-Kasulu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kasulu Mhandisi Godfrey Kasekenya, amefungua Mradi wa ujenzi wa madarasa mawili pamoja na ofisi ya Mwalimu mkuu katika shule ya Msingi Nyakasanda iliyopo  kata ya Nyachenda wilayani hapa.

Mradi huo uliogharimu zaidi ya Shilingi Mil 15/ umezinduliwa leo tarehe 21.11.2018 katani hapo, ambapo fedha zilizotumika kutokana na thamani ya nguvu pamoja na  michango ya wananchi ni jumla ya shilingi 10,018,600.  na kiasi cha Shilingi  5,750,000 kimetoka katika Fedha za Mfuko wa Jimbo.

Akiongea na  watumishi pamoja na wananchi waliojitokeza katika ufunguzi huo, Mhandisi Kasekenya amesema kuna masuala ya utekelezaji yanawezekana kutelekezwa na wananchi pale watakapoweza kusikilizana na kukubaliana kufanya kazi za maendeleo kwa pamoja wakitumia nguvu na fedha kidogo pamoja na kuishirikisha Serikali.

Amesema kuwa kuendana na hali halisi ya mahitaji ya Shule hiyo, bado kuna upungufu wa vyumba vya madarasa 15, nyumba za walimu 8, matundu ya vyoo 32, madawati 121. Wilaya itatoa msaada wa vifaa vya kiwandani pale ambapo nguvu za wananchi zitatumika na itaonekana kuna uhitaji wa Halmashauri kusaidia katika ukamilishaji wa miundo mbinu hiyo ya Elimu.

amesisitiza  wakazi hao na jamii kwa ujumla kuongeza kasi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na utengenezaji wa madawati. “Kutokana na mfumo wa Elimu bure, kuna tarajio la uwepo wa wanafunzi wengi watakaohitimu  Elimu ya Msingi na kujiunga na Kidato cha kwanza. Hali hii itapelekea hitajio kubwa la miundombinu hiyo ifikapo mwaka 2021” amesisitiza Kasekenya.

Ametoa  Rai kwa wazazi kusitisha kuwatuma watoto wa kike kwenye  masoko ya jioni au usiku na kuwapunguzia kazi za nyumbani ambazo  hupelekea kuwashusha kitaaluma. “Utaratibu huo ndio chanzo cha Ajira ndogondogo za mitaani, aidha hupelekea watoto wengi kujikuta wakijiingiza katika tabia zisizofaa na hata kupelekea kupata mimba za utotoni” amesisitiza Mkurugenzi.

Amewaasa wakazi hao kuhakikisha wanaitunza Miundombinu hiyo ya kielimu. Aidha amesisitiza wazazi kufuatilia maendeleo ya kitaaluma na kuwahimiza watoto wao kuhudhuria shuleni kwa ufasaha huku wakishirikiana na walimu ili kutokomeza utoro wa rejareja na ule wa kudumu ambao ni chanzo cha kudidimia kwa  Taaluma yao.

Diwani wa Kata ya Nyachenda Mh. William Luturi amemshukuru Mkurugenzi kwa ahadi yake kwa niaba ya Serikali kuhusu kusaidia umaliziaji wa Miradi inayotekelezwa na wananchi. Aidha amempongeza kwa uhimizaji, ushauri na usimamizi mzuri wakati wa ujenzi wa Miundombinu hiyo ya elimu “Mbegu uliyoipanda matunda yake yataonekana baada ya muda mfupi ujao kwani kwa Jicho la haraka hatuwezi kuiona faida yake kwa sasa ila baada ya kitambo kifupi tu. Mungu akujalie uendelee kuwepo  ili na wewe ujionee Matunda ya kazi yako” amesema Luturi.

“Ujenzi huu tumeufanya kwa kuchangishana kwa hiyari ambapo kila kaya ilichangia shilingi 4000, pamoja na kutumia akiba ya matofali ya kijiji yaliyokuwepo kwa muda mrefu. Fedha zilizobaki tumezielekeza katika ujenzi wa Ofisi ya ulinzi ambao unaendelea kufanyika. Hii ni katika kuhakikisha tunaweka mazingira ya kijiji na kata  katika hali ya usalama pia”amesisitiza Luturi.

Luturi ameushukuru uongozi wa kijiji pamoja na wananchi kwa kufanya kazi bila ugomvi wala kusukumana. Aidha amewasisitiza kuendelea kutekeleza miradi mingine ya Maendeleo kwa nguvu na umoja ili kutimiza malengo waliyojiwekea katika kuhakikisha wanatekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo katani hapo.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • KASULU DC YAANZISHA SHAMBA DARASA LA VIAZI LISHE KUKABILIANA NA UTAPIAMLO

    June 15, 2025
  • KUU KASULU YAKAGUA MIRADI YA MWENGE

    June 13, 2025
  • MATUMIZI YA ZANA ZA UFUNDISHAJI YATAJWA KUONGEZA UFANISI SHULENI

    June 11, 2025
  • WALIMU SHULE YA MSINGI KISUMA WATOA SHUKRANI KWA WADAU WALIOCHANGIA SARE NA VIFAA KWA WANAFUNZI

    June 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.