Serikali imeiwezesha Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kiasi cha shilingi bilioni 1.60 kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye robo ya kwanza katika mwaka wa fedha 2024/2025.
_
Hayo yamebainishwa leo Alhamisi Novemba 14,2024 na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Mhe. Eliya Kagoma kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani robo ya kwanza kilichofanyika katika Ukumbi wa Kagoma makao makuu ya halmashauri hiyo.
_
Amesema fedha hizo zitatatua changamoto mbalimbali za miundombinu pamoja na kusogeza karibu huduma za kijamii kwa wakazi wa eneo hilo kitu kitakachosaidia ustawi wao kuimarika.
_
"Natoa wito kwa madiwani muhakikishe mnapa ushirikiano Mkurugenzi kwa kuhakikisha usimamizi wa karibu wa fedha hizo unafanyia katika kata zenu pamoja na kuwaelimisha wananchi juu ya miradi mbalimbali inayotekelezeka kwenye maeneo yenu," amesema.
_
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu,Dkt.Semistatus H. Mashimba amesema fedha hizo kiasi cha shilingi milioni 700 zitatumika kununua vifaa tiba katika sehemu zinazotoa huduma za afya na zingine zitahusika kwenye ujenzi wa shule ya sekondari katika Kijiji cha Mgombe na ile ya msingi katika Kijiji cha Kacheli.
_
Awali akizungumza katika tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Kasulu,Mhe. Kanali Isaac Mwakisu ameipongeza halmashauri hiyo kwa nguvu waliyoiweka ya kuandikisha wapiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hadi kufikisha 117% kitu kilichosaidia mkoa kushika nafasi ya sita kitaifa.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.