Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Mhe.Thobias Andengenye leo Jumapili Septemba 22,2024 amefunga mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka 2023.
_
Tukio hilo limefanyika katika Shule ya Sekondari ya Bogwe wilayani Kasulu na kuhusisha viongozi,makundi maalum na wadau mbalimbalu mkoani humo.
_
Tofauti na makundi hayo pia waudhuriaji wengine walikuwa Naibu Waziri TAMISEMI,Mhe. Zainab Katimba,Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma,Hassan Rugwa,wakuu wa wilaya wa mkoa huo,Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali,wakurugenzi wa halmashauri,viongozi wa vyama vya siasa pamoja na madhehebu ya dini.
Akizungumza katika tukio hilo Andengenye amesema kuwa lengo la Serikali ya Awamu ya Sita ni kuongeza uelewa, uwazi na kupanua wigo wa matumizi ya Sensa ya Mwaka 2022 katika kupanga mipango jumuishi kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi na kimazingira
Aidha, amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo kupitia kitengo cha Mawasiliano serikalini na Teknolojia ya Habari kuhakikisha matokeo hayo yanaweka katika tovuti zote za halmashauri ili kusaidia wananchi kupata taarifa hizo Kwa urahisi ili kuutangaza Mkoa Kwa wadau
Naibu waziri OR-TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba amesema kuwa wanatambua umuhimU wa matokeo ya sensa ambayo usaidia katika kupanga maendeleo kwa kuangalia sehemu za kuongeza nguvu.
Na kuongeza kuwa nchi inapoelekea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 matokeo hayo yatasaidia kuwaongoza kupata vituo na vifaa vinavyohitajika katika uchaguzi husika.
Kwa upande wake Afisa Takwimu Mwandamizi Omary Mdoka amezitaka Halmashauri kutumia matokeo hayo ili kuakisi mahitaji ya wananchi wanao wahudumia ili kusadia kuboresha ukusanyaji wa mapato.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.