Na.Andrew Mlama.
Waziri Mkuu Kasim Majaliwa (MB) amefanya ziara mjini kasulu ambapo amepokelewa na kuzungumza na wakazi wa maeneo mbalimbali ya mji na wilaya ya Kasulu.
Akizungumza na wakazi hao, waziri Majaliwa amewataka wananchi kuendelea kuwaamini viongozi wao katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi unaofanywa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh.Rais John Pombe Magufuli.
Ameeleza kuwa, Serikali haitosita kuwachukulia hatua watumishi wa umma walio wazembe na kuwataka wahakikishe wanatumia siku tatu kati ya tano za kazi kwa kwenda maeneo walipo wananchi ili kuwasiliza na kutatua kero zao pamoja na migogoro badala ya kushinda ofisini.
Amesisitiza kuendelea kuboresha huduma ya maji katika mji wa Kasulu kutokana na kukua kwa kasi na kuhitaji huduma hiyo kwa kiasi kikubwa na uhakika. Aidha utekelezaji wa kurekebisha miundo mbinu ya barabara za mji kwa kiwango cha lami, zenye urefu wa km 6 unaendelea.
Amesema suala la usambazaji wa umeme, Serikali imedhamiria kila nyumba ya mtanzania itapata umeme kwa kupunguza gharama za uwekaji huduma hiyo toka Shilingi 380,000 mpaka 27,000 tu. Aidha Amesisitiza kutoendelea kwa gharanma za kulipia nguzo za umeme ambapo amefafanua kuwa jukumu hilo litabebwa na serikali sio mwananchi.
Amewataka wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama kushirikiana na taasisi zinazohusika kudhibiti mipaka ili kuzuia wimbi la wahamiaji haramu kutoka nchi ya Burundi wanaoingia nchini kinyume na sheria pia kuingiza silaha. Udhibiti huo ufanyike kwa wafanyabiashara pia ili walipe ushuru wanapotoa na kuingiza bidhaa nchini.
Waziri mkuu ameahidi kurudi mkoani hapa tarehe 30.09.2018 ili kufuatilia utekelezaji wa maagizo yake pia kuzunguukia wilaya ambazo hajazitembelea ili kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali hususani wilaya ya kasulu vijijini, Kibondo na Kakonko.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.