Na Mwandishi Wetu
Wajasiriamali katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wamepongezwa kutokana na ubunifu mbalimbali walioufanya katika sekta ya kilimo ulioenda kubadilisha maisha ya watu.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Mhe. Dkt. Khamis Mkanachi alipotembelea banda la halmashauri hiyo ambaye leo alikuwa mgeni rasmi katika maonesho ya Nanenane Kanda ya Magharibi ambapo aliwawakilisha wakuu wote wa wilaya wa ukanda huo.
“Nimeona teknolojia na nguvu kubwa iliyowekwa katika tasnia ya kilimo baada ya kupita katika mabanda mbalimbali kwa maana ya kumasidia mkulima niwapongeze wenzangu wa Kasulu kwa kuja na vitu vilivyoonekana havina maana lakini vikiweza kutumika vizuri vinaweza kubadilisha maisha ya watu ,” amesema.
Aidha, ametoa wito kwa halmshauri hiyo kumshika mkono mbunifu wa mbolea za asili za Nigarofu Organics na Nigafosi Booster, Ibrahim Mnigambogi zinazotengenezwa kupitia mabaki ya mimea mingine kwa kuleta matokeo chanya kwenye upandaji na ukuzaji wa mazao.
“Mimi nashauri tu mbunifu huyu aweze kusaidiwa na halmsahuri yake kwenye kuitangaza bidhaa yake ili wakulima wengi waweze kuitumia,changamoto kubwa inayotukabili wengi wetu ni kufikiri vitu tunavyoletewa kutoka sehemu nyingine na kuuzwa bei ghali ndio vina ubora na kuacha kuvikubali vyetu vya asili,” amesema.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.