• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

VIONGOZI WATAKIWA KUHIMIZA WAZAZI KUPELEKA WATOTO KUANZA KIDATO CHA KWANZA

Posted on: January 8th, 2024

 Na Mwandishi Wetu

Wenyeviti wa vijiji, watendaji wa kata  pamoja na viongozi wa dini  katika Halamshauri ya Wilaya ya Kasulu wametakiwa kuhimiza wazazi    kuhakikisha wanawapeleka watoto  kijunga na kidato cha kwanza.

Hayo yamebainishwa mapema hii leo wilayani humo na Afisa Elimu Taaluma (Sekondari) wa halmashauri hiyo, Mussa Kanyoe   alipopita kukagua mapokezi ya wanafunzi hao na kubainisha kuwa wanafunzi wote watapokelewa hata kama hawajakamilisha baadhi ya vitu na maandalizi mengine yatafanyika  wakiwa tayari shuleni.

“Lengo ni watoto wafike mapema na kuanza kujifunza kwa pamoja na si kufika taratibu kwasababu kuchelewa kufika shuleni kutasababisha watoto wengine wasiwe vizuri kitaaluma,” amesema.

Amesema ataendelea kupita mashuleni kuhakikisha wale wote waliopata nafasi  wanaanza masomo huku akifuraishwa kwenye baadhi ya shule alizopita kwa namna wazazi walivyoandamana na watoto kwenda kuwasajili.

 Afisa Elimu Kata ya Titye, Yoab Henyura amebainisha kuwa watahakikisha wanatoa matangazo kwa kupita kila kijiji   ili wazazi waweze kuleta watoto wajiunge na kidato hicho.  

“Mtoto aletwe shuleni vyovyote vile atakavyokuwa kama hana sare au mkoba anatakiwa aje shule ili aanze masomo hivyo vitu vingine makubaliano yetu ni kwamba mzazi ataendelea kutafuta polepole,” amesema.


Mmoja wa wazazi aliyemleta mwanaye katika Shule ya Sekondari ya Nkundusi,Fadhila Kabuyanga aliishukuru serikali kwa namna ilivyofanya maandalizi mazuri ya kuwapokea watoto na kuwataka wazazi wengine kuhakikisha wanawapeleka watoto kupata elimu.


Naye Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Rungwe Mpya, Elton Ntazina amesema kuwa waraka wa serikali umeainisha mwanafunzi kuanza masomo bila masharti yeyote na wako tayari kuwapokea ili lengo hilo lipate kutimia.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • PAMBA KUINUA UCHUMI WA WAKULIMA

    May 08, 2025
  • WASHIRIKI WA MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA WAHASWA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    April 29, 2025
  • MAWAKALA WA VYAMA KURUHUSIWA KITUONI KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

    April 29, 2025
  • MAWAKALA WA VYAMA KURUHUSIWA KITUONI KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

    April 29, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.