Na. Andrew Mlama.
Ukarabati wa Miundombinu ya maji katika kata za Rusesa na Kwaga unatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Ukarabati huo unatokana na uharibifu wa miundombinu ya maji uliofanywa na Mkandarasi anayefanyakazi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Kidahwe mpaka Kasulu mjini.
Mabomba yakiwa kwenye lori tayari kwa kushushwa ili utendaji kazi uanze mara moja. Mabomba hayo yamehifadhiwa katika Kituo cha afya Rusesa.
Diwani wa kata ya Kwaga Mh. Baraka Mkuyu, amethibitisha kupokelewa kwa mabomba 620 ambayo yatatumika katika kurudishia mfumo huo ulioharibiwa.
“Kero ya upatikanaji wa Maji safi katika kata ya Kwaga imekuwa ni ya muda mrefu hivyo ukarabati huu utakapokamilika utaamsha ari ya maendeleo kwa wananchi wa kata hii.” alisema Mkuyu.
Nao wananchi wa kata ya Kwaga wameushukuru uongozi wa Kata hiyo pamoja na Halmashauri kwaujumla kwa kuhakikisha ukarabati huo unafanyika na huduma ya maji inarejea katani hapo.
“Tumekuwa na changamoto ya upatikanaji maji safi pia wanawake na watoto wamekuwa wakitumia muda mwingi kufuata maji mtoni.” walisema wakazi wa kata ya Kwaga.
Ulazwaji wa mabomba na taratibu za kiufundi zinatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa ili huduma hiyo muhimu iweze kurejea tena katani hapo.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.