• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

UJENZI WA KITUO CHA AFYA MAKERE NI UTEKELEZAJI WA AZMA YA MAMA SAMIA YA KUSOGEZA HUDUMA ZA AFYA KARIBU

Posted on: April 4th, 2025

UJENZI WA KITUO CHA AFYA MAKERE NI  UTEKELEZAJI WA AZMA YA MAMA SAMIA YA KUSOGEZA HUDUMA ZA AFYA KARIBU

Na Mwandishi Wetu 

Ujenzi wa Kituo cha Afya Makere kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma utakaogharimu kiasi cha Sh.Bil. 2.62 ni utekelezaji wa azma ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inayotaka kupanua wigo wa huduma za afya ili wananchi wasiende mbali kuzifuata huduma hizo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu (Kazi Maalum),Mhe. George Mkuchika amebainisha hayo leo wilayani humo alipofanya ziara ya kutembelea mradi huo unaotekelezwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ikiwa ni sehemu yake ya kurudisha kwa jamii zilizopo kwenye utekelezaji  wa ujenzi wa barabaraba inayotoka eneo la Kabingo hadi Buhigwe.

“Kwahiyo magonjwa mengi mliyokuwa wakati mwingine mnakwenda kuyatafutia tiba Hospitali ya Wilaya sasa huduma hizo mtazipata hapa…lakini umati kuwa mkubwa hivi inaonyesha mnakingoja kwa hamu na niwapongeze kwa kupata kituo kama hiki ambacho kinatoa huduma zote za hospitali mpaka upasuaji utakuwa unafanyika,” amesema.

Pia,amewataka wananchi wa wilaya hiyo kujianda na mradi mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ambao mkataba wake umesainiwa kwa kipande cha kutoka Tabora hadi nchini Burundi kwakuwa utafungua fursa nyingi za ajira  hasa kwa vijana pamoja na kuimarisha suala zima la uchumi.

Katika hatua nyingine  Mkuchika ameiasa jamii kuitunza amani iliyopo kwakuwa Serikali imehakikisha imedhibiti mianya yote ya uhalifu wilayani humo  ambapo hadi hivi sasa hali imekuwa shwari.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kasulu,Mbelwa Chidebwe amesema kuwa wilayani humo wanatembea vifua mbele kwakuwa vitu vyote walivyovinadi kwenye kampeni za uchaguzi uliopita tayari vimevitekeleza kwa kiasi kikubwa.

Mmoja wa waudhuriaji wa tukio hilo,Everin Reuben amempongeza  Mhe. Rais  kwa  jitihada zake za kusogeza huduma za afya karibu  pamoja na kutimiza azma yake ya kumtua mama ndoo kichwani na kumtaka Waziri Mkuchika kumfikishia salamu hizo.

Ikumbukwe pindi mradi huo utakapokamilika utahusisha jengo la utawala,kichomea taka,nyumba ya mtumishi,maabara,jengo la wazazi na upasuaji,chumba cha kuhifadhia maiti pamoja na idara ya wagonjwa wa ndani.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • PAMBA KUINUA UCHUMI WA WAKULIMA

    May 08, 2025
  • WASHIRIKI WA MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA WAHASWA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    April 29, 2025
  • MAWAKALA WA VYAMA KURUHUSIWA KITUONI KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

    April 29, 2025
  • MAWAKALA WA VYAMA KURUHUSIWA KITUONI KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

    April 29, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.