Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, wakijadili jambo baada ya kutembelea na kujionea hali halisi ya utekelezaji wa Mradi wa Skimu ya umwagiliaji katika Kata ya Rungwempya.
Na.Andrew Mlama.
Wakulima katika kata ya Rungwempya iliyopo wilayani hapa, waepuke Kilimo cha kutegemea mvua za msimu na badala yake waelekeze nguvu zao katika Kilimo cha umwagiliaji kwa kuitumia Skimu ya umwagiliaji iliyopo katani hapo.
Kilimo cha umwagiliaji hufanyika wakati wote wa mwaka bila kuathiriwa na wingi, uchache au kutokuwepo kabisa kwa mvua. Mfumo mzuri wa usambazaji maji ambapo kuna mifereji yenye jumla ya urefu wa mita 3400 inayogawanya maji mashambani, inapelekea sehemu kubwa katika eneo la bonde lenye ukubwa wa Hekta 125 lililopo katani hapo kupata maji wakati wote.
Ikumbukwe, aina hii ya Kilimo ni ya kisasa na humuhakikishia mkulima mavuno kwani mara nyingi mazao yanayolimwa katika bonde hilo ni yale ya muda mfupi ambayo hutumia mwezi 1 hadi 4 kukomaa na kuwa tayari kwa kuvunwa. Mpunga, Mahindi na mbogamboga ni sehemu ya mazao hayo ambapo kila mkulima akiweka mkakati mzuri atajihakikishia kuongeza kipato chake kupitia kilimo hicho.
Uwepo wa maji ya uhakika katika eneo hilo, umeruhusu shughuli nyingine za maendeleo ambazo zinafanywa na wananchi ikiwemo ufugaji wa kisasa wa Samaki.
Halmashauri ya wilaya ya Kasulu na Serikali kwa ujumla imelipa kipaumbele suala la kilimo cha umwagiliaji ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yameathiri kwa kiasi kikubwa mwenendo wa mvua nchini kote.
Utunzaji wa Mazingira hasa ulinzi wa vyanzo vya maji, utapelekea ufanisi mkubwa katika aina hii ya Kilimo. Shime wakazi wa Kata ya Rungwempya, wakati ndio huu kwani ipatikanapo fursa tuonyeshe mabadiliko ambapo kwa kufanya hivyo tutakua tunaunga mkono juhudi za Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ili kufikia malengo ya Tanzania ya Viwanda.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.