Serikali imetenga eneo lenye ukubwa wa hekta 4446 kutoka katika italu cha wanyamapori na kuziingiza katika Kijiji cha Kagera Nkanda kwa ajili ya kuwahamisha wananchi waliopo eneo oevu la kitongoji cha Katoto
-
Hayo yamebainishwa jana na Mkuu wa Wilaya ya kasulu, Mhe. Kanali Isaac Mwakisu alipofanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kagera Nkanda
"Ni ubinadam mkubwa na wa hali ya juu sana kupatiwa hekta 4446 ambazo ni sawa na ekari 10, 986 kwa wananchi wa Kagera Nkanda kwa ajili ya kuhamisha wananchi wa Katoto ambao walikua wanakaa kilomita 75 kutoka makao makuu ya kijiji," amesema Mwakisu
Aidha, Mwakisu ameagiza wananchi kwa kushirikiana na Halamashauri ya Kijiji hicho kupanga matumizi bora ya ardhi ili kusaidia kupunguza migogoro ya ardhi.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Emmanuel Ladislaus ameshauri wananchi hao kutenga eneo kubwa kwa ajili ya huduma za kiserikali hasa huduma za afya ili ziweze kusogea karibu
-
"Ninawaomba mtumie akili za ziada katika kufanya mipango bora ya ardhi hii mliyopewa kwa kutenga eneo kubwa kwaajili ya taasisi za kiserikali hasa kituo cha afya", amesema.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kasulu, Mbelwa Chidebwe amewataka viongozi wa eneo hilo kuzingatia suala la uadilifu kwenye kutunza na matumizi ya eneo hilo kwa kuwapatia wananchi kama ilivyokusudiwa.
-
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.